IJUE Biblia

IJUE Biblia Kufundisha Neno la Mungu. Follow this link to join my WhatsApp group: https://chat.whatsapp.com/CHdc

ZAMANI TUKIWA WADOGO NILIKUWA NASIKILIZA NYIMBO ZA KWAYA MBALIMBALI, MOJA YA KWAYA NILIYOSIKILIZA SANA NI KINONDONI REVI...
12/02/2026

ZAMANI TUKIWA WADOGO NILIKUWA NASIKILIZA NYIMBO ZA KWAYA MBALIMBALI, MOJA YA KWAYA NILIYOSIKILIZA SANA NI KINONDONI REVIVAL KWAYA, WIMBO WANGU PENDWA ULIKUWA ULE ‘MTU WA NNE’.

•Siku moja kanisani kwetu tuliambiwa ATAKUJA MHUBIRI MGENI kutuhudumia, tukaambiwa ni MMOJAWAPO WA WAIMBAJI WA KWAYA YA KINONDONI REVIVAL, nikafurahi nikahitaji kumwona uso kwa uso mwimbaji wa kwaya ninayoipenda sana.

•Kweli, alikuja Mtumishi wa Mungu Maikos Mbwete, akatuhudumia KWA NENO LA BWANA. Alihubiri ujumbe ambao sitausahau, kichwa cha ujumbe kilikuwa “ROHO YA UWEZA”, Kutoka kwenye kitabu cha Isaya 11:2.

•Miaka mingi baadaye, nimeshakua mtu mzima; ninaandika jumbe mbalimbali huku mitandaoni, Mtumishi wa Mungu Maikos alinitafuta, akajitambulisha kwa jina nikamwambia NAKUKUMBUKA, ULIKUJA KANISANI KWETU KUTUHUDUMIA KWA NENO LA MUNGU.

Kutokea pale tukawa tunawasiliana mara kadhaa.

Jambo ambalo nilikuwa silijui kuhusu maisha yake, ni kwamba YEYE NA MKE WAKE HAWAKUWAHI KUPATA MTOTO.

-MWAKA HUU NI MWAKA WA 21, TANGU WAOANE MWAKA 2004 WALIKUWA HAWAJAPATA UZAO,

LAKINI MUNGU AMEWAKUMBUKA KWENYE MAJIRA YAKE, MWAKA HUU AMEWAPA MAPACHA!.

•MUNGU AMEIFUTA AIBU YAO, AMEONDOA HUZUNI YAO, AMEWASHANGAZA KWA KUAMUA KUFUTA MATUSI NA KEJELI.. AMEWAPA WATOTO WAWILI KWA PAMOJA.

•NILIPOONA USHUHUDA WAO, KWANZA NILISHANGAA KISHA MOYO WANGU UKAJAA FURAHA NA SHUKURANI KWA MUNGU!.

•NIMETIWA MOYO KWAMBA, HATA MAMBO UNAYOONA YAMECHELEWA MUNGU ANAWEZA AKAYAKAMILISHA KWA WAKATI WAKE.

•HAWA WATUMISHI WA MUNGU WANASHUHUDIA WANASEMA, KWA MIAKA YOTE HIYO PAMOJA NA KUTUKANWA, KUSEMWA NA KUDHIHAKIWA SANA HAWAKUWAHI KUWAZA KUMWACHA YESU, KWENDA KWA WAGANGA WALA KUCHEPUKA.. WALIENDELEA KUMWAMINI YESU NA KUIWEKA IMANI YAO KWA MUNGU!.

•MIAKA 21 NI UMRI WA KIJANA MTU MZIMA AMBAYE ANGEWEZA KUWA CHUO KIKUU SASA.. LAKINI WALIVUMILIA.

•NINACHOWEZA KUKWAMBIA KATIKA YALE UNAONA MUNGU AMEKAWIA KWAKO, USIMWACHE YESU, USIONDOE IMANI YAKO KWA MUNGU. ATAKUKUMBUKA, ATAFANYA!.

HONGERENI SANA Mr. & Mrs. Maikos Mbwete. YESU AENDELEE KUTUKUZWA KUPITIA NINYI.

Jina la Yesu LITUKUZWE!.

Shalom

_Mwl. Nick_
0712265856
(WhatsApp #)

09/02/2026

“K**A SARA ANGEKUWA TASA WA UMRI MDOGO K**A MIAKA 25 HADI 35, ANGELIAMINI KWA HARAKA SANA LILE NENO LA MUNGU ALILOPEWA KWAMBA ATAKUMBATIA MWANA MWAKA UNAOFUATA!.

•LAKINI KWASABABU ALIPITA DESTURI, KIBINADAMU ILIKUWA HAIWEZEKANI TENA; NDIO MAANA ALICHEKA, HUKU AKIJUA HAKUNA KINACHOWEZA KUTOKEA!!.

•UMRI WALA DESTURI ZENU HAZIMZUII MUNGU KUFANYA YALE ALIYOYAKUSUDIA KUYAFANYA, MAZINGIRA YAKO MAGUMU HAYAMZUII MUNGU KUFANYA YALE ALIYOYAPANGA KWA AJILI YAKO;

HAKUNA MAJIRA, DESTURI WALA KANUNI NA TARATIBU ZINAZOWEZA KUZUIA UTENDAJI KAZI WA MUNGU ANAPOTAKA KUFANYA JAMBO LAKE, MWAMINI YEYE, LIAMINI NENO LAKE; NENO LAKE NI AMINA NA KWELI, HATA K**A MAZINGIRA YAMEKATAA!!”.

_Mwl. Nick_
+255712265856
(WhatsApp #)/

JE, UMEANDIKWA JINA LAKO KATIKA KITABU CHA MBINGUNI??.Ndugu yangu moja ya jambo la msingi kabisa kwa ustawi wa Roho yako...
21/08/2025

JE, UMEANDIKWA JINA LAKO KATIKA KITABU CHA MBINGUNI??.

Ndugu yangu moja ya jambo la msingi kabisa kwa ustawi wa Roho yako sio kufurahia majina yako kuandikwa ukutani au vitabu vya starehe za dunia hii.

Yesu aliwaambia wanafunzi kwa Luka 10:20 kuwa "Wasifurahi kwa kuwa pepo na kuzimu zinawatii, Bali wafurahi kwa kuwa majina yao yameandikwa mbinguni"!

Yesu hakukurupuka kusema maneno haya, anajua mtu akiwa hajaandikwa katika kitabu za mbinguni huyo ni hasara na ni wakutupwa motoni.

Ufunuo wa Yohana (Rev) 20:15 Na iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto.

Ndugu yangu jitahidi sana majina yako yaandikwe katika kitabu cha mbinguni.

Majina yako yanaandikwaje????

Majina yako yanaandikwa hivi.

1. Amua kutubu kabisa maovu yako mbele za Mungu kwa moyo wako wote.

2. Amua kabisa kubadilisha mfumo wote wa maisha yako, Anza kuhudhuria ibada za kweli katika makanisa ya kipentekoste bila kutegea wala kuruka ibada.

3. Amua kuacha kwenda katika sehemu ambazo ndio zinakupelekea kuwa muovu na kuzidi kumkosea Mungu.

4. Amua kupata marafiki wapya wenye uelewa na wanao mpenda Mungu, hiyo itakusaidia kudumu kwa Mungu na kuzidi kulitunza jina lako katika kitabu cha Mungu.

K**a jina lako halijaandikwa katika kitabu cha Mungu unao wajibu wa kuamua leo kumfuata na kumrudia Mungu kwa njia ya Toba ya kweli.

Nakusalimu katika pendo la Yesu Kristo.

Ev. Joseph Kidifu Jr.

Sikia kilichomvuta Yesu Kristo kuja duniani sio uzuri wa vilivyopo dunia wala mali na vitu vya anasa vilivyoijaza dunia....
20/08/2025

Sikia kilichomvuta Yesu Kristo kuja duniani sio uzuri wa vilivyopo dunia wala mali na vitu vya anasa vilivyoijaza dunia.

Bali kilichomvuta Yesu Kristo kuja duniani ni wingi wa dhambi duniani na watu kujikita zaidi kwenye mambo yaliyo kinyume na mapenzi na makusudi ya Mungu.

Ndio maana mtu mwenye dhambi anapotubu dhambi na kurudi kwenye kuyaishi mapenzi ya Mungu, Mungu hufurahi na kumuwekea ulinzi usio na mfano.

Mungu anasubiri mtu mmoja anayejijua ni mdhambi na anahitaji kusamehewa na Mungu ili amsemehe na ndio kazi kuu ya Yesu Kristo ni kuwarudisha watu katika njia njema impasayo kuiishi.

Haikuwa vigumu kwa yule mwizi pale msalabani aliyetundikwa pamoja na Yesu kusamehewa mara baada ya kujua yeye ni mwenye dhambi na anamhitaji Mungu, katika maumivu makubwa pale juu ya msalaba lakini Yesu Kristo bado alimuambia yule Mwizi AMESAMEHEWA DHAMBI ZAKE.

Unajua nini???

YULE MWIZI ALIYETUBU JUU YA MSALABA NDIO MTU WA KWANZA KUINGIA UZIMANI KWA TOBA WAKATI YESU HAJAKATA ROHO PALE MSALABANI.

HIYO NI UTHIBITISHO TOSHA KUWA YESU KRISTO ANATUPENDA WENYE DHAMBI NA TUKIFUNGUA VINYWA VYETU NA KUTUBU DHAMBI ZETU KWA KUMAANISHA ANATUSAMEHE NA KUTUPA MWANZO MPYA WA MAISHA YETU.

KUTUBU INAKUHUSU WEWE, KUTUBU INAKUPA NAFASI YA KUBADILIKA NA KUANZA UPYA NA MUNGU.

Ev. Joseph Kidifu Jr

01/08/2025

“MWEZI HUU UJIDHATITI KWA AJILI YA MAMBO YALIYOKUFA KWENYE MAISHA YAKO!.

_Anaandika Mwl. Nickson Mabena_

KUFA KWA JAMBO LOLOTE KUNAWEZA KUSABABISHWA NA MENGI YAKIWEMO;-

1. JAMBO KUZALIWA KABLA YA WAKATI WAKE.

-Mtoto akizaliwa NJITI, kuna maarifa ya ziada hufanyika ili kuweza kuyaokoa maisha yake. Kuna mambo huwa yanazaliwa ‘NJITI’ kabla ya wakati wake, ukikosa JITIHADA na MAARIFA YA KUYAFANYA YAISHI UJUE YANAWEZA YAKAFA!.

•Jaribu kuwaza juu ya JAMBO LAKO, HALIKUZALIWA NJITI? HALIKUTOKA KABLA YA WAKATI WAKE? HUENDA LILIKUFA SABABU ULILIZAA KABLA YA WAKATI.

2. KUULIWA NA ADUI.

•Shetani anaitwa MWIVI, yeye anazo kazi k**a tatu; KUIBA, KUCHINJA na KUHARIBU.

‭Yn 10:10 SUV‬
[10] Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele.

•Utaona MOJA YA KAZI YAKE NI KUCHINJA. Kuna jambo la KIMUNGU lilizaliwa kwako, kisha baadaye LIKAFA; usijue kumbe HUYU MWIVI AMELICHINJA KABISA!.

•YEYE HUWA ANAZUIA JAMBO LA MUNGU KUZALIWA, NA LIKIZALIWA ANATAFUTA NAMNA YA KULICHINJA KABISA.

Yule Mwanamke kwenye UFUNUO 12, Biblia inasema alipokuwa anataka KUZAA; JOKA lilikuwepo pale ili KUHAKIKISHA ANAMLA MTOTO.

•Jambo lile lililokuwa limekufa kwako, HALIJALIWA NA JOKA?.

•UNAPASWA KUWA NA IMANI YA KWAMBA; JAMBO LOLOTE LILILO-KUFA LINAWEZA KUFUFULIWA. USILIKATOE TAMAA WAZO LAKO, HUDUMA YAKO, MAISHA YAKO, NDOA YAKO INAWEZA KUFUFULIWA TENA!.

UNAJUA KWANINI?

1. MUNGU ANAO UZOEFU WA KUFUFUA YALIYOKUFA!.

•Biblia inasema SISI TULIKUWA WAFU KWA MAKOSA NA DHAMBI ZETU. Kwa lugha rahisi TULIKUWA TUMEKUFA.

‭Efe 2:1 SUV‬
[1] Nanyi mlikuwa wafu kwa sababu ya makosa na dhambi zenu;

•Lakini MUNGU HAKUTUKATIA TAMAA, HAKUTUACHA TUKIWA WAFU; KWA KUPENDA KWAKE MWENYEWE AKATUFUFUA;

‭Efe 2:6 SUV‬
[6] Akatufufua pamoja naye, akatuketisha pamoja naye katika ulimwengu wa roho, katika Kristo Yesu;

•MUNGU ANAO HUO UZOEFU WA KUFUFUA VILIVYO-KUFA!.

Nikufunulie zaidi?

“UKITAKA KUJENGA IMANI NA TUMAINI JUU YA JAMBO FULANI UNALOTAKA MUNGU AKUTENDEE, ANGALIA JE! KUNA WATU WENGINE AMEWAHI KUWATENDEA? ANGALIA KUNA SHUHUDA ZA WALIOWAHI KUTENDEWA? UKISHAPATA, UWE NA HAKIKA NA WEWE ANAWEZA KUKUTENDEA PIA!”.

•KWAHIYO K**A MUNGU AMEWAHI KUFUFUA, BILA SHAKA NA JAMBO LAKO ANAWEZA KULIFUFUA PIA, BILA SHAKA NA KITU CHAKO ANAWEZA KUKIHUISHA PIA;

•MUNGU HUWA ANA KAWAIDA YA KURUDIA KILE ALICHOWAHI KUFANYA, UNAJUA KWAMBA WAKATI MUSA ANAKUTANA NA BAHARI YA SHAMU, ANGETAFAKARI VIZURI ANGEKUMBUKA KWAMBA MUNGU HUWA ANAGAWANYA(GA) MAJI; UNAKUMBUKA WAKATI WA UUMBAJI? ALIYAGAWA MAJI, Kwahiyo kwa Musa hakikuwa kitu kipya na kigeni. Baada ya Musa, unakumbuka Yoshua na Mto Yordani?.

•NAKUOMBEA KWA MUNGU AKUFANYIE KILE UMESIKIA AMEWAHI KUWAFANYIA WENGINE KATIKA JINA LA YESU!.

•K**A MUNGU ALIKUFUFUA WEWE UKIWA MFU, ATASHIDWA DUKA LAKO? ATASHINDWA KAZI YAKO? ATASHINDWA MRADI WAKO? HAWEZI KUSHINDWA!.

2. ROHO MTAKATIFU ANA KAZI YA KUHUISHA VILIVYOKUFA!.

•Ona hapa anahuishi MIILI.

‭Rum 8:11 SUV‬
[11] Lakini, ikiwa Roho yake yeye aliyemfufua Yesu katika wafu anakaa ndani yenu, yeye aliyemfufua Kristo Yesu katika wafu ataihuisha na miili yenu iliyo katika hali ya kufa, kwa Roho wake anayekaa ndani yenu.

•Biblia inasema HUYU ROHO MTAKATIFU, NDIYE ALIYEMFUFUA YESU KATIKA WAFU!.

•NI JAMBO LIPI SASA NI LA KUMSHINDA?

•Unaukumbuka ule MTO kwenye Biblia, Ezekieli 47? Kasome vizuri hiyo sura uyaone maajabu yake.

•HUU MTO, ANATAJWA ROHO MTAKATIFU HAPO; ANGALIA HIKI ANACHOKIFANYA;-

‭Eze 47:9 SUV‬
[9] Tena itakuwa, kila kiumbe hai kisongamanacho, *kila mahali itakapofika mito hiyo, kitaishi;* kutakuwapo wingi mkubwa wa samaki, kwa sababu maji haya yamefika huko maana *maji yale yataponyeka*, na *kila kitu kitaishi po pote utakapofikilia mto huo.*

•Kila KIUMBE KITAISHI
•Maji yale HATAPONYEKA
•Kila KITU (Weka kitu chochote) KITAISHI POPOTE UTAKAPOFIKILIA MTO HUO.

•ROHO WA MUNGU ANAPOKUWEPO, ANAPOINGIA, KITU CHOCHOTE KINAWEZA KUISHI TENA!.

•Hata ILE NDOTO YAKO, HATA ILE KAMPUNI YAKO, hata MAISHA YA MAOMBI, hata NDOA au DUKA... ROHO WA MUNGU ANAWEZA KUHUISHA TENA, ROHO WA MUNGU ANAWEZA KUFUFUA TENA.. NIKUSIKIE UKINENA KWA LUGHA MPYA!!!!!!.

JIDHATITI, MRUHUSU ROHO WA UFUFUO AFANYE MAAJABU YAKE KWENYE MAISHA YAKO NDANI YA MWEZI HUU..

BWANA YESU AWE PAMOJA NA WEWE!.”

*HAPPY NEW MONTH*

Shalom, Shalom.

_Mwl. Nick_
0712265856
(WhatsApp #)

09/10/2024

“NATAMANI SANA KUONA ILE NGUVU TULIYOKUWA TUNAITUMIA KWENYE MAMBO YA ANASA, DHAMBI NA DUNIA HII TUITUMIE KUBWA ZAIDI KWENYE MAMBO YA MUNGU NA UTUMISHI TULIOPEWA!.

•KABLA YA KUOKOKA: ULISAFIRI KUFUATA MATAMASHA YA MUZIKI, ULILIPA PESA NYINGI KWA AJILI YA KIUINGIA KLABU, ULITONGOZA WANAWAKE KWA BIDII, ULIKESHA BAR BILA KULALAMIKA, ULIWANUNULIA WATU POMBE, ULIHONGA WANAWAKE na MAMBO MENGINE MENGINE MENGI.

Ninategemea BAADA YA KUOKOKA;-

USAFAIRI SANA KWA AJILI YA MIKUTANO YA INJILI, SEMINA NA MAKONGAMANO YA MAOMBI, KUTOA PESA ZAKO KWA AJILI YA KAZI YA MUNGU, KUWASHUHUDIA WATU HABARI NJEMA ZA YESU, KUKESHA KANISANI KWENYE MAOMBI NA IBADA, KUMTUMIKIA MUNGU NA KUTOA SADAKA BILA MALALAMIKO.

HAPO KWANZA TULIYAFANYA YALE YOTE SABABU TULIKUWA WAFU, HATUKUWA TUNAJUA WALA HATUKUMJUA BWANA NA MWOKOZI WETU YESU. LAKINI KWAKUWA TUMESHAOKOKA, TUMEMJUA BWANA BASI TUVITOE VIUNGO VYETU NA MIILI YETU KWA BWANA KWA NAMNA ILE ILE NA ZAIDI ILI KUMZALIA MUNGU MATUNDA!!.

”Warumi 6:19
[19]Nasema kwa jinsi ya kibinadamu kwa sababu ya udhaifu wa miili yenu. Kwa kuwa k**a mlivyovitoa viungo vyenu vitumiwe na uchafu na uasi mpate kuasi, vivyo hivyo sasa vitoeni viungo vyenu vitumiwe na haki mpate kutakaswa. ”

Shalom, Shalom!.

_Mwl. Nick_
0712265856
(WhatsApp #)

Mungu anapokupa maelekezo halafu usiyafanye kwa vitendo yale maelekezo hana kitu kingine cha kukusaidia.Eliya aliambiwa ...
22/04/2024

Mungu anapokupa maelekezo halafu usiyafanye kwa vitendo yale maelekezo hana kitu kingine cha kukusaidia.

Eliya aliambiwa atoke aende sarepta kwa mama mjane, lakini angeamua kubaki pale angekufa kwa njaa maana Mungu alishamaliza siku za Eliya kuhudumiwa na kunguru. Hata usafiri wa kuondoka pale kando ya mto hakupewa bali aliambiwa aondoke hapo.

Ibrahim mwenyewe aliambiwa aondoke katika nchi ya baba yake tena Ibrahim aliambiwa mpaka atakaoambiwa hakupewa hata uelekeo k**a alivyopewa Eliya.

Lakini kwa Imani Ibrahim alifuata maelekezo ya Mungu, ukuu wako na mafanikio yako vinategemea vile unamsikia Mungu na kutii kwa vitendo yale maelekezo aliyokupa Bwana.

Ukiyapiga teke matendo nakuambia kwa jina la Yesu Kristo hautapiga hatua yoyote kwenye maisha yako na kwenye huduma yako.

Mafanikio yako na ustawi wako umefungwa kwenye kusikiliza maelekezo kutoka kwenye kinywa cha Mungu na kuyatekeleza kwa vitendo na sio kwa maneno ya midomoni.

VITENDO VIMEBEBA HATUA ZAKO ZA KUOGEZEKA.

Nakusalimu kwa jina la Yesu.

Ni kwa amani tu.

Ev. Joseph Kidifu Jr
Kutoka Bethel.
0755438142

1 Mambo ya Nyakati 12:22 Maana siku kwa siku humjia Daudi watu wa kumsaidia, hata wakapata kuwa jeshi kubwa, k**a jeshi ...
16/03/2024

1 Mambo ya Nyakati 12:22 Maana siku kwa siku humjia Daudi watu wa kumsaidia, hata wakapata kuwa jeshi kubwa, k**a jeshi la Mungu.

Yesu Kristo asifiwe sana watu wa Mungu.

Kuna neno hapo "Watu wa kumsaidia"

Kwenye maisha kuna vita fulani huwezi kuishinda peke yako, utahitaji watu wa kukusaidia ili ushinde hiyo vita.

Unaweza ukawa unavuka mipaka fulani kwenye maisha yako lakini kila hujawahi kufanikiwa, basi unahitaji watu wa kukusaidia kuvuka eneo hilo.

Wako watu wa kukusaidia wamefichwa ili ubakie hapo hapo au hivyo hivyo.

Watu wa kukusaidia kwenye biashara zako, uchumi wako, huduma yako na mambo mengine...

Muombe Mungu akuletee watu wa kukusaidia ili uvuke.

Nakusalimu mbarikiwa wa Mungu.

Ev. Joseph Kidifu Jr
Kutoka Bethel
0755438142

WAZO LAKO NI MLANGO WA MUUJIZA WAKO.Marko  5:28 maana alisema, Nikiyagusa mavazi yake tu, nitapona.Sikia mtu wa Mungu, l...
12/03/2024

WAZO LAKO NI MLANGO WA MUUJIZA WAKO.

Marko 5:28 maana alisema, Nikiyagusa mavazi yake tu, nitapona.

Sikia mtu wa Mungu, lile wazo unalopata uwapo katika hali ya mapito au huzuni, uwapo katika tafakari ya namna gani ya kutoka katika hali uliyoichoka hilo wazo ndio limebeba mlango wa muujiza wako.

Huyu mama aliwaza moyoni mwake kwamba akigusa pindo la vazi la Yesu Kristo atapata jibu la hitaji lake.

Kile unachokisumbukia kwa muda mrefu, majibu yake Mungu alishayapitisha katika mawazo yako, amini yale mawazo ambayo Mungu aliyapitisha kwako, iamini ile sauti iliyokupa maelekezo ya namna ya kufanya ili utoke katika hali unayopitia.

Mama huyu aliamini ile sauti iliyomuambia akigusa atapona, ataiweka katika matendo, akaamua kuinuka kumtafuta Yesu Kristo alipo huku anayo ajenda yake kwa siri na alipofanya hivyo tu alipona msiba wake.

Kwa jina la Yesu Kristo na wewe uinukapo na kuitii ile sauti aliyoipitisha Mungu ndani utapona na kutoka kwenye mateso yako.

Ile sauti iliyokuambia nenda katoe yule kuku awe sadaka, iamini ile hiyo sauti imebeba funguo za miujiza kwako.

Ile sauti iliyokuambia nenda katoa kale kafedha kwa mtumishi fulani nenda katoe hiyo sauti imebeba mpenyo wako.

Ile sauti iliyokuambia nenda kaombee jambo fulani, usiipuze nenda hiyo sauti imebeba funguo za mlango wako wa baraka.

Kornelio hakubeza ile sauti iliyomuambia atume watu wakamfuate mtumishi wa Mungu Petro, ile sauti ilibeba wokovu wa nafsi yake na watu wa nyumbani mwake.

MATENDO YA MITUME 10 sura yote.

Bathoromayo aliposikia Yesu Kristo anapita, hakujiamulia kuita tu, ile imani yake ndani ikampa mzigo wa kuita na kuita kwake kukampa muujiza wa kuona.

Isipuuzie lile wazo, hilo wazo ni limeleta majibu ya maombi yako ya muda mrefu.

Inuka uwe mtendaji wa kila unachosikia ndani yako katika jina la Yesu Kristo.... Ameeen.

Ev. Joseph Kidifu Jr
Kutoka Bethel.
0755438142

Address

Tabora

Telephone

0755438142

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when IJUE Biblia posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Establishment

Send a message to IJUE Biblia:

Share