Mwenebato

Mwenebato INFOMATION Contact me +255755484041

Karibu sana wapendwa hii si yakukosa . Njoo upate Burudiko la kweli
11/12/2019

Karibu sana wapendwa hii si yakukosa . Njoo upate Burudiko la kweli

KOO KUU ZA WABEMBEKwa mujibu wa Wazee wa Lubunga za kibembe koo kuu za kibembe ni 7; Mzee Shile au katika simulizi nying...
25/10/2019

KOO KUU ZA WABEMBE
Kwa mujibu wa Wazee wa Lubunga za kibembe koo kuu za kibembe ni 7;
Mzee Shile au katika simulizi nyingine Ik**a Sungu alimzaa Mzee Shile au Leka na Mzee Mbondo,
Mzee Mbondo akazaa wana saba(7) k**a ifuatavyo;
Wasimkuma (Bashim'uma); Baadhi ya Wazee husema huyo ndiyo mtoto mkubwa wa mzee Mbondo.

Wasik**akulu (Bashi'amakulu);

Wasimkinji (Bashim'inje); Hawa shina lao la Ufalme linatokea Lwindi/Itombwe na ndiyo Wafalme wakubwa wa nchi ya Wamasanze pale Baraka.

Wasimwenda (Bashimwenda); hawa waliwahi kutoka mapema itombwe na asili ya Bwami yao ni "Bwami bwa e'ombo" na Mlima wao wanashirikiana na Waziba na Watwa.

Wabungwe; Hawa wengi ndiyo Wanaangukia Ng'anza na ndiyo walimeza zaidi Wagoma.

Wasimnyaka (Bashimnyaka);

Wasisango (Bashisango);

Ukoo wa 8 k**a ule wa Wasikalangwa(Bashi'alangwa) una utata na wazee wengi wa koo zingine husema ni ukoo wa Kinyindu au kitwa.
Ukoo wa Kisimwenda uko pia Uregani.
Ukoo wa "Bashiatabi" ni Wazyoba-Wamasanze siyo Wabembe.
Ukoo wa Baciba "Waziba" ni Kikabila cha Wagoma na mila yao yote ni ya Ki-goma ingawa wana baadhi ya mila za kitwa pia, hii hutokana na koo zingine za Wazyoba kuingiliana na Watwa vile wa mwanzo kukutana na watwa katika mwambao.

PICHA: Mwami Kisasu IV Mfalme wa Wasimkinji.
'oka_ya_Babondo

 Wagoma, Ba'ôma, Bagoma ni kabila la kimanyema kutoka Kigoma, asili yake mtambazo wa magharibi wa ziwa Tanganyika kwa mk...
04/10/2019


Wagoma, Ba'ôma, Bagoma ni kabila la kimanyema kutoka Kigoma, asili yake mtambazo wa magharibi wa ziwa Tanganyika kwa mkabala sawa na mji wa ujiji na kigoma, urefu wa zaidi ya maili 70 ilikuwa ndiyo nchi ya Goma kwa upande wa DRC.

Mji wao wa asili katika Ujiji ni Kigoma-Mjini, kuja k**ini hadi katosho na burega, halafu ng'ambo ya luiche kuambaa mwambao kasaba, kaseke, kisha katika mkoa wa rukwa maeneo ya utinta, msamba, kipili na kisiwa cha manda, msimulizi anatueleza kwamba jina 'Burega' (ni jina la Babu wa Babu wa Abdul Nondo), miji ya Wagoma kihistoria ni vifungo "enclaves" kwasababu ya kuhamahama kwa shughuli za uvuvi na miji ya Kigoma-k**ini ilianza k**a miji ya kikambi na baadae wengi walirudi Ujiji.

Lusambo ambapo sasa panaitwa Shede au Kigedeko ndipo Wagoma walipofikia na maeneo yao mengine ni pamoja na Bangwe-Burega mpaka ujiji, Wazee wa kabila la 'Waha' wengi wao walikuwa ni wakulima, na wazee wa Kabila la Wagoma wao shughuli zao ilikuwa ni uvuvi na utengenezaji wa mitumbu ambapo biashara ilikuwa ikifanyika baina yao kwa kubadilishana bidhaa za mazao na uvuvi. Msimulizi anatueleza yakwamba kutokana na ukarimu waliokuwa nao wazee wa pande zote mbili wazee wa kiha walikuwa wakitembeleana na wagoma, ''Tugende kwa Bhagoma' (Twende kwa wagoma) ni maneno ambayo waha walikuwa wakizungumza, na ndiko jina Kigoma lilikopatikana. haswa wakimaanisha eneo lile la Kigoma Mjini.

Msimulizi anatueleza kwamba mji wa ujiji ulifahamika tangu karne ya 9.
Mfalme wa Wagoma alifahamika k**a 'Sultan Simba' ambae alikuwa ni mkarimu na mpenda undugu.

Ukoo mkubwa wa Wagoma ni 'Wene mbago' "Bene mba'o" ambapo wengine hudhani ni lakabu ya Wagoma wote, lakabu ya Wagoma "Ba'oma bakatan(d)a...", Ndugu zao katika asili ni Wabuyu, Waluba (Katanga) na Wazoba kiujumla ijapo wengi wengine ni Wapwa wa Wang'anja.

Msimulizi anatueleza kwamba, kwa dini Wagoma wa Ujiji takribani wote ni waislamu.
Lugha yao ni Kigoma ijapo hakizungumzwi kila siku kutokana na matumizi ya kiswahili kwasababu ya historia ya biashara ya utumwa na muingiliano na waarabu tangu karne 19. Kwasasa lugha ya Kigoma kinazungumzwa na watu wachache sana huko ujiji maeneo ya Kazaroho na baadhi ya maeneo ya Kabondo na Majengo, hii ni kutokana kwamba makabila yote ya kimanyema yaliacha mila zao za 'MWAMI SING' na 'BAMI PLU' na makabila yote ya Kimanyema yalijikita katika uzungumzaji wa lugha ya kiswahili, na ndio maana mara nyingi 'waha' hupenda kuwaita wamanyema 'Waswahili' sababu kubwa ni hiyo.

02/08/2019
Mwanza mwanza ni jpili tu
29/07/2019

Mwanza mwanza ni jpili tu

26/07/2019
It’s not what goes into your mouth that defiles you; you are defiled by the words that come out of your mouth.” Matthew ...
26/07/2019

It’s not what goes into your mouth that defiles you; you are defiled by the words that come out of your mouth.”

Matthew 15:11

Our words have power! Our words are a reflection of the state of our hearts. If our hearts are filled with bitterness then unkind words are likely to come from our mouths. If we are discouraged, negativity is likely to be found in our conversations. Conversely, if we want to live joyful and holy lives our words must be filled with kindness, patience, and love.

SIBWESA, MCHANGANI,Moja ya kijiji kinachopatikana k**ini mwa Kigoma, kijiji hichi kipo jirani na hifadhi ya taifa ya Mah...
20/07/2019

SIBWESA, MCHANGANI,
Moja ya kijiji kinachopatikana k**ini mwa Kigoma, kijiji hichi kipo jirani na hifadhi ya taifa ya Mahale, kwa upande wa k**ini kimepakana na Kalya, na pia kipo katika mwambao wa ziwa Tanganyika., kijiji hichi kina rasi ya maajabu iliyozungukwa na majabari ya mawe, rasi hii imechongoka kuelekea mashariki mwa Congo ambapo mabaharia wengi wa ziwa Tanganyika hutumia rasi hii k**a alama moja wapo ya kupata muelekeo waendako, upepo wa k**i unapovuma (Rukuga) mabaharia huegesha vyombo vyao vya usafiri katika kijiji hichi ili kuukwepa upepo kwasababu rasi hiyo haipitiki wakati wa upepo mkali, kutokana na hilo serekali imeamua kujenga bandari ndogo kwenye fukwe ya kijiji hichi ambapo meli kutoka Congo, Zambia na Kigoma zitaweza kuegesha hapo,

Msimulizi anatueleza kwamba kijiji hichi kinaaminika kwa kuwepo na mazindiko ya nguvu za giza kwakuwa kuna moto usiozima nyakati za usiku kutoka upande wa rasi hiyo, ambapo ukijiaribu kuusogelea moto huo hautaukuta lakini ukiwa mbali unauwona. Vilevile msumilizi anaeleza maajabu ya jogoo anaewika katika rasi hiyo jambo ambalo muwiko huo wa jogoo hupelekea wavuvi kuvua samaki na dagaa kwa wingi, Kijiji hichi ndio kinasifika kwa kutoa samaki wa mapambo wenye gharama kubwa, katika miaka ya 1990 meli kongwe ya MV Liemba ilikuwa ikionekana ikifanya safari zake wakati wa usiku maeneo ya kijiji hichi wakati kiuhalisia meli hiyo inakuwa imeegesha bandari ya Kigoma. Wakazi wa kijiji hichi ni kabila la Wagoma-Wamanyema ambao wapo katikati ya kijiji (Mchangani), Waha wanapatikana mashariki (Makola) na Wafipa wanapatikana eneo la rasi hiyo (Rasini)..

Kutokana na uwepo wa Jogoo huyo wakazi wa Mchangani waliipa jina 'Jogoo FC' timu yao mpira, Upande wa Makola ambapo Waha hupatikana wao Timu yao ya Mpira waliipatia jina 'Makola Rangers FC' kwakuwa upande wao ndio unaopakana na msitu wa hifadhi ya taifa ya Mahale, na upande huu wa Rasini kutokana na moto wenye kutoa nuru isiozima waliamua kujiita 'Rasini Stars FC'' Maajabu huonekana uwanjani timu hizi za mpira zinapokuwa zikipambana kijijini hapo,

HISTORIA YA MJI WA TABORA NA UPATIKANAJI WA JINA LA TABORA.Tabora ni moja ya mkoa unaopatikana upande wa magharibi mwa n...
15/06/2019

HISTORIA YA MJI WA TABORA NA UPATIKANAJI WA JINA LA TABORA.

Tabora ni moja ya mkoa unaopatikana upande wa magharibi mwa nchi ya Tanzania. Ni miongoni mwa mkoa mkubwa nchini Tanzania. Ukiwa mkoani Tabora unaweza kufika kwenye wilaya zenye historia na vivitio vya utalii k**a wilaya ya Sikonge, Uyui, Urambo, Nzega, Kaliua, Igunga Na Manispaa Ya Tabora Mjini.

makabila yanayopatikana mkoani Tabora ni Wanyamwezi ambao ndio wenyeji huku makabila k**a Wasukuma, Waha na makabila mengine wakiwa k**a wageni. Ukitoka mkoa wa Dar Es Salaam, kuna umbali wa kilomita zaidi ya 800 kufika mkoani Tabora. Na unaweza kufika mkoani Tabora kwa usafiri wa mabasi, ndege na treni. Wakazi wa mkoa huu wanalima sana tumbaku na baadhi ya mazoa ya chakula na biashara.

Pia kuna wafugaji ambao hufuga k**a sehemu ya biashara na tamaduni. Hali ya hewa ni nzuri ambapo kuna joto kiasi kipindi cha kiangazi na hali ya ubaridi kipindi cha masika. Wakazi wa Tabora hupendelea sana vyakula k**a viazi, wali na ugali huku wakitumia sana karanga k**a sehemu ya kiungo cha mboga. Pia mkoani Tabora kuna matunda ya aina mbalimbali yenye kupendwa na wakazi wa mji wa Tabora.

Na mara baada ya kufahamu machache kuhusiana na mkoa wa Tabora, ni wakati sasa wa kufahamu historia ya asili ya jina Tabora. Ifahamike kwamba, katika miji mingi iliyopo hapa barani Afrika asili ya majina yao yametokana na uwepo wa lugha za kikabila na baadhi ya miji majina yao yametokana na ujio wa wageni. K**a ilivyo katika historia ya mji wa Mtwara kuwa asili ya jina hilo linahusiana sana na lugha ya kimakonde.

Na hata kwa upande wa Tabora asili ya jina hilo linahusiana sana na lugha ya kinyamwezi. Historia inasema hivi wakati Waarabu wanafika katika mji wa Tabora mnamo miaka ya 1830 walikuta mji huo umeendelea hasa katika maeneo ya Kwihala na Itetemya. Na hii ni kwa sababu kuwa, maeneo hayo yalikuwa yana idadi kubwa ya watu.

Waarabu hawakuwa na mpango wa kukaa hapo, ila kwa kuwa walirazimishwa kutoa kodi na ndipo walipoaanzisha vita na mwisho kuchukua maeneo hayo na kujenga tembe ambalo lipo pale mpaka leo.

Na mara baada ya Waarabu kukaa hapo, kuliibuka baadhi ya Waarabu ambao waliokuwa maarufu sana k**a wakina Kazeh. Na Kwa kuwa mtu huyo kumwakilisha Sultani wa Zanzibar, alitokea kuheshimiwa sana na wakazi wa Tabora.

Na hata yale maeneo aliyokuwa anakaa yalijulikana k**a kwa Kisehi (jina lilitamkwa kimakosa). Na mpaka wamishionari na wapelezi wanafika katika mji wa Tabora k**a wakina Dr.livingstone na Henry Stanley waliufahamu mji wa Tabora kwa jina la kwa Kisehi ambapo kwa Waarabu alifahamika k**a Kazeh. Hivyo mji wa Tabora ukafahamika k**a Kazeh kulingana na ujio wa wageni hao.

Lakini ikumbukwe kuwa utamaduni wa wenyeji kwa wakati ule na hata sasa, ulikuwa unategemea sana kilimo cha viazi vitamu. Baada ya kuvunwa viazi hivyo vinachemshwa na kisha kukatwa vipande na kuanikwa. Zao litakalopatikana baada ya mchakato huo linajulikana kwa kinyamwezi k**a matobolwa. Hivyo mwingiliano wa Wanyamwezi, Waarabu pamoja na Waswahili kutoka Pwani ndio kulileta ugeuzi wa matamshi hayo kutoka “matoborwa” “matohorwa” na kuwa Tabora. Hivyo neno Tabora limetokana na kushindwa kimatamshi kwa baadhi ya wageni .

Hivyo wengi walianza kusema, “twendeni kwenye mji wa matoholwa” na mwisho wa siku binadamu anaamua kurahihisha matamshi na kuwa “twendeni Tabora” na hivyo ndivyo jina Tabora lilivyopatikana. Na leo hii ukiwa mjini Tabora utapata k**ikia sehemu panaitwa “Kazeh hill” wakimaanisha sehemu ambayo liwali Kazeh alipokuwa anakaa.

Leo hii Tabora ni moja ya mkoa wenye kubeba historia kubwa sana, ukizungumzia historia ya TANU huwezi kuacha kutaja mji wa Tabora. Na pia mkoa wa Tabora ni moja ya mkoa wenye vivutio vingi sana, kuna makumbusho ya Kwihala, kuna misitu ya asili,kuna mabonde na milima yenye kuvutia, kuna mito mbalimbali na bila kusahau ukiwa wilayani Sikonge kuna kaburi la mchungaji wa kwanza wa kinyamwezi wa kanisa la Moraviani.

Na pia utapata kuona kanisa la pili la Moraviani lililojengwa miaka ya 1897 na linatumiaka mpaka leo. Lakini pia utalii wa kiutamaduni unapatikana sana mkoani Tabora hasa kwa makabila k**a Wanyamwezi na Wasukuma. Hakika mkoa wa tabora ni urithi wetu. Maandiko haya ni sehemu tu ya historia ya Tabora, bado mawazo yako yanahitajika sana.


Address

ILEMELA
Mwanza

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Mwenebato posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share