Story Za Kusisimua za Dizo tz

Story Za Kusisimua za Dizo tz Usipo jituma utatumwa

26/07/2026

STORY.....LAZIMA NILIPE KISASI
MTUNZI......Mr dekechu
WhatsApp....... 0689311780

SEHEMU YA 1

Neema alikuwa ni msichana mpole sana alikuwa ni binti mwenye heshima ambaye alikuwa anapendwa na kila mtu kuanzia shuleni hadi mtaani na alikuwa ni mtu wangu wa karibu sababu tulikuwa majirani alipokuwa anaishi Shangazi yangu na nyumbani kwao hakukuwa na umbali
Kuna siku wakati tupo njiani tumetoka shule Neema aliniuliza "hivi Coxian ww ni mwenyeji wa wapi na wazazi wako wanaishi wapi??
Nikamjibu"mimi ni mwenyeji wa Arusha na huko ndipo walipokuwa wanaishi wazazi wangu japo kwa bahati mbaya kwa sasa hawapo duniani ndo maana huyu shangazi yangu alinichukua nije kusoma huku Dar es salaam"
Nilivyomjibu hivyo Neema akaguna akatulia kidogo nilivyomuangalia usoni nikaona ameanza kutoa machozi nikamuuliza"vipi wangu mbona unalia?
Akanijibu"yani ulivyoongelea swala la kufiwa kwa wazazi wako wote wawili umenipa sana machungu na mtu yyte akiongelea swala la kifo lazima machozi yanidondoke sababu mimi pia ni yatima sina Baba wala Mama na pale ninapoishi nalelewa na Bibi yangu tu yeye anajishughulisha na kilimo ili mimi nisome roho inaniuma sana Coxian na wazazi wangu wamekufa kifo ambacho siji kukisahau lakini lazima nilipe kisasi labda sio mimi"
Neema aliongea hayo maneno kwa uchungu huku akimwaga machozi hadi nikajikuta na mimi machozi yameanza kunidondoka nikamuambia "basi nyamaza usilie Neema ni mapenzi ya mungu tu ameamua kuwachukua wazazi wetu ipo siku na sisi tutafuata"
Nilijitahidi kumbembeleza Neema hadi akanyamaza akatulia kabisa lakini kuna kitu bado nikawa nataka kukijua kutoka kwake alivyoniambia hatokuja kusahau kifo cha wazazi wake lazima alipe kisasi lakini nikawa nasita kumuuliza nilihofia anaweza akaanza kulia
Wakati nafikiria jinsi ya kuanza kumuuliza yeye ndo akaniuliza swali ambalo nilitaka kumuuliza aliniuliza "kwani Coxian ww wazazi wako walikufa kwa kuumwa au kwa ajali hebu nielezee ilivyokuwa??
Nikamjibu"walikufa kwa kuumwa wangu na ww je hebu nielezee kwann umeniambia hutokuja kukisahau kifo cha wazazi wako na lazima ulipe kisasi??
Nilivyomuuliza hivyo Neema akaniambia "Coxian ni stori ndefu sana kwa mda huu mimi siwezi kukusimulia baadae ukija nyu
bani kusoma tutatafuta sehemu iliyotulia nitakusimulia kila kitu wangu"
Neema alivyonijibu hivyo nikatulia lakini nilitamani hata anisimulie mda ule sema tu mimi nilikuwa tayari nimeshafika nyumbani yy akawa anaendelea na safari
Niliagana na Neema nikaingia ndani nikabadili nguo nikala harakaharaka nikaanza kufanya kazi za pale nyumbani ambazo nilikuwa nazifanya kila nikirudi shule
Nilimaliza kazi nikaoga nikajiandaa nikachukua vitabu vyangu safari ya kwenda nyumbani kwakina Neema ikaanza ile siku sikuwa na lengo lakwenda kusoma nilikuwa na mzuka wa kujua kifo cha wazazi wa Neema kilikuwaje hadi anasema lazima alipe kisasi

Inaendelea

Address

Njenga
Mtwara

Telephone

+255689311780

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Story Za Kusisimua za Dizo tz posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Establishment

Send a message to Story Za Kusisimua za Dizo tz:

Shortcuts

Share