29/11/2025
Yesu Kristo ni Bwana wa mabwana, mtawala, ana miliki mbingu na vyote vilivyomo, dunia na vyote vilivyomo, chini ya nchi na vyote vilivyomo. Hakuna na hatakuwepo k**a huyu Mwamba.
Ufunuo 5
9 Nao waimba wimbo mpya wakisema, Wastahili wewe kukitwaa hicho kitabu na kuzifungua muhuri zake; kwa kuwa ulichinjwa, ukamnunulia Mungu kwa damu yako watu wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa,
10 ukawafanya kuwa ufalme na makuhani kwa Mungu wetu; nao wanamiliki juu ya nchi.
11 Nikaona nikasikia sauti ya malaika wengi pande zote za kile kiti cha enzi, na za wale wenye uhai, na za wale wazee, na hesabu yao ilikuwa elfu kumi mara elfu kumi na elfu mara elfu,
12 wakisema kwa sauti kuu, Astahili Mwana-Kondoo aliyechinjwa, kuupokea uweza na utajiri na hekima na nguvu na heshima na utukufu na baraka.
13 Na kila kiumbe kilichoko mbinguni na juu ya nchi na chini ya nchi ya juu ya bahari, na vitu vyote vilivyomo ndani yake, nalivisikia, vikisema, Baraka na heshima na utukufu na uweza una yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na yeye Mwana-Kondoo, hata milele na milele.
14 Na wale wenye uhai wanne wakasema, Amina. Na wale wazee wakaanguka, wakasujudu.
Huyu MWAMBA hakuna falme, mamlaka na chochote kijiinuacho chaweza kumkabili, akishuka kuzimu mapepo yote na mkuu wao wanasarenda na kupooza.
Yeyote aliye na njaa na aje kwake, atashibishwa. Yeye aliyekiu aje anywe maji, maji ya uzima bure.