Makutano Tv

Makutano Tv To educate, inform, entertain and inspire community through the power of online content.

Wamiliki wa makao ya watoto na vituo vya malezi ya watoto (Day Care) Mkoa wa Iringa wamekutana kwa pamoja kwa lengo la k...
19/09/2026

Wamiliki wa makao ya watoto na vituo vya malezi ya watoto (Day Care) Mkoa wa Iringa wamekutana kwa pamoja kwa lengo la kuzungumza kwa lugha moja, kubadilishana uzoefu wa malezi na makuzi ya watoto, pamoja na kuunda uongozi utakaosimamia umoja wao.

Akizungumza katika kikao hicho kilichofanyika September 18 2026 katika Ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mwenyekiti wa Umoja wa Wamiliki wa Makao ya Watoto Taifa, Evance Tegete, amesema lengo la kikao hicho ni kuwaunganisha wamiliki wa makao ya watoto, kubadilishana uzoefu kuhusu malezi na makuzi ya awali ya mtoto, pamoja na kujadili umuhimu wa kuwa na uongozi imara.

Tegete amesema uongozi huo utasaidia kuwaunganisha wamiliki wa makao ya watoto nchini, ambao kwa sasa wanafikia takribani 500,
ili waweze kuwa na mfumo wa pamoja wa kushughulikia changamoto zinazowakabili katika kutoa huduma za malezi.

Amesema umoja huo pia utashirikiana na Serikali katika kuhakikisha watoto wanapata ulinzi na usalama, hususan watoto wanaoishi mitaani, wanaofanyiwa ukatili majumbani na wale wanaolelewa katika familia ambazo usalama na ustawi wao unaweza kuwa hatarini.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Umoja wa Wamiliki wa Makao ya Watoto Mkoa wa Iringa, Jane Hussen Mwalembe, aliyechaguliwa kuongoza umoja huo, amesema atahakikisha anawaunganisha wamiliki hao ili kuwa na umoja imara na unaoweza kuwasaidia kujitegemea kiuchumi.

Mwalembe amesema kujenga umoja huo kutawawezesha wamiliki kushirikiana katika kuboresha huduma wanazozitoa na hatimaye kuhakikisha watoto wanaowahudumia wanapata malezi bora na mazingira yanayosaidia ustawi wao.

Naye Mwenyekiti wa Day Care Mkoa wa Iringa, Fanikisha Peter, amesema moja ya changamoto kubwa inayojitokeza ni kuibuka kwa vituo vya malezi ya watoto vinavyoanzishwa bila waendeshaji kuwa na elimu na taaluma inayohitajika katika malezi ya watoto.

Amesema kutokana na changamoto hiyo, wamekuja na mkakati wa kuwa na viongozi katika kila kata ambao watasaidia kubaini vituo vinavyoanzishwa bila kuzingatia taaluma ya malezi ya watoto.

Kwa upande wake, Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Iringa, Martine Chuwa, amewataka wamiliki wa makao ya watoto kuhakikisha wanatoa malezi na huduma zinazolenga ustawi wa mtoto badala ya kuishia kuwahifadhi watoto pekee.

Chuwa amewataka wamiliki hao kutumia wataalamu wa ustawi wa jamii waliopo katika kata zao pale wanapokutana na changamoto zinazohusu watoto, akisisitiza kuwa maafisa hao wana ujuzi wa kutoa ushauri na mwongozo kuhusu malezi na ustawi wa watoto.

Amesema malezi ya watoto yanahitaji kujitoa na kufanya kazi kwa wito, akisisitiza kuwa watoto wanahitaji ulinzi, usalama na mazingira yanayowawezesha kukua katika hali bora.

“Malezi ya watoto si siasa hakikisheni mnafanya kazi hiyo kwa wito, kwa kuwa watoto hao ni wa Mungu,”
amesema Chuwa.

Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Iringa, Martine Chuwa, amesema kuwa kwa sasa wazazi wameendelea kuonesha mwitikio mkubwa k...
18/09/2026

Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Iringa, Martine Chuwa, amesema kuwa kwa sasa wazazi wameendelea kuonesha mwitikio mkubwa katika uanzishwaji wa vituo vya kulelea watoto mchana, hali inayosaidia kuhakikisha watoto wanapata malezi na uangalizi unaostahili, sambamba na kupunguza vitendo vya ukatili dhidi yao.

Amesema kuwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa pekee, kuna jumla ya vituo takribani 14 vya kulelea watoto mchana, vinavyolenga kuwapa watoto mazingira salama wakati wazazi wakiendelea na shughuli zao za kila siku.

17/09/2026

SOS CHILDRENS VILLAGES YAWAFIKIA VIJANA 30 WILAYA YA KILOLO KATIKA AFUA YA UZAZI NA UCHUMI ENDELEVU

Vijana wapatao 30 wamefikiwa na SOS Childrens Villages katika afua ya afya ya uzazi na stadi za maisha kwa uchumi endelevu katika Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa.

Afisa Mradi katika masuala ya afya ya uzazi na stadi za maisha Jesca Kawonga kutoka SOS amesema kuwa mafunzo hayo kwa waelimishaji rika yametekelezwa katika Wilaya ya Mufindi na kuhitimishwa Wilaya ya Kilolo yaliyodumu kwa siku mbili.

Naye Roda Kunzugala Mratibu wa afya ya uzazi na mtoto kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo ameeleza lengo la kuwapa elimu vijana ili iwe rahisi kuwafikia wengine kwani vijana wamekuwa wakipenda kupewa elimu na vijana wenzao pia ameendelea kusema kuwa wamefanikiwa pia kuanzisha kilabu za masuala ya afya ya uzazi kwa shule za shekondari ili kupambana na kukomesha mimba za utotoni kwani watoto hao wakipata mimba katika umri mdogo via vyao vya uzazi huwa bado havijakomaa pia wanakuwa hawana elimu ya kutosha kuhusu masuala ya malezi sahihi kwa mtoto.

Rhoda amesema pia jitihada za kukomesha mimba za utotoni zimeanzia kwa watoto wa miaka 10 hadi 19 na inashauriwa kijana kuweza kubeba ujauzito ni kuanzia miaka walau 20 kwenda juu.

Halmashauri ya Manispaa ya Iringa imeendelea kuimarisha uanzishwaji wa vituo vya kulelea watoto wadogo mchana kupitia Pr...
17/09/2026

Halmashauri ya Manispaa ya Iringa imeendelea kuimarisha uanzishwaji wa vituo vya kulelea watoto wadogo mchana kupitia Programu Jumuishi ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto, PJT MMAM Lengo likiwa kuwawezesh a wazazi kushiriki katika shughuli za uzalishaji mali bila kuwa na hofu juu ya usalama, malezi na ustawi wa watoto wao.

Hapa ni Ndiuka, Kata ya Igumbilo, Manispaa ya Iringa ambapo Mkurugenzi wa Halmashauri Ya manispaa Bi Zaina Mlawa ametoa Majengo Mawili katika Shule ya Msingi Ndiuka yanayotarajiwa kubadilishwa kuwa kituo cha kijamii cha kulelea watoto mchana, kitakachohudumia watoto wapatao 250.

Mpango huu unalenga kuwawezesha wazazi kuendelea na shughuli zao za kila siku huku watoto wakiwa katika mazingira salama na yenye huduma za malezi, makuzi, elimu na lishe na hapa wazazi wanaeleza.

Kwa upande wake, Afisa Ustawi wa Jamii Kanda ya Ruaha Bi Getrude Tilphone Mbena anaeleza hatua zilizochukuliwa katika uibuaji na uanzishwaji wa vituo vya kijamii, ikiwemo kuwafikia watoto wanaohitaji huduma hizo ni 80 sambamba na kituo cha Matulila Day Care kimefanikiwa kutoa watoto 45 kuanza darasa la awali kati ya watoto 65.

Zaina Abas Lehani kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Iringa pamoja na kumshukuru Mkurugenzi. ameeleza kuwa utekelezaji wa Programu Jumuishi ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto umeleta matokeao kwa kuhakikisha kila kata inakuwa na kituo cha kijamii cha kulelea watoto mchana.

IRINGA:  Kata ya Kwakilosa Mtaa wa Samora yamefanyika maadhimisho ya LisheMe 4, ke 29 na watoto 36Elimu: ulaji wa chakul...
10/09/2026

IRINGA: Kata ya Kwakilosa Mtaa wa Samora yamefanyika maadhimisho ya Lishe
Me 4, ke 29 na watoto 36

Elimu: ulaji wa chakula bora, chakula cha mtoto miezi 6.

Wahusika: CDO, watendaji wa Mitaa,CHW's, Mwenyekiti wa Mtaa Samora, Wazazi

KATA - KIHESA MTAA - SOKONI SIKU YA AFYA NA LISHE YA MTAA:Huduma zilizotolewa ni pamoja na wa hali ya lishe@ Upimaji wa ...
10/09/2026

KATA - KIHESA
MTAA - SOKONI

SIKU YA AFYA NA LISHE YA MTAA:

Huduma zilizotolewa ni pamoja na
wa hali ya lishe
@ Upimaji wa magonjwa yasiyo ya kuambukizwa
@ utoaji wa vyandarua
za minyoo
A
kinga vya malaria
kwa vitendo na elimu mbalimbali kutoka kwa wataam.

KATA -  GANGILONGA MTAA - WILOLESISIKU YA AFYA NA LISHE YA MTAA:Huduma zilizotolewa  na wataalam1. Elimu2. Upimaji wa ha...
10/09/2026

KATA - GANGILONGA
MTAA - WILOLESI

SIKU YA AFYA NA LISHE YA MTAA:
Huduma zilizotolewa na wataalam

1. Elimu
2. Upimaji wa hali ya lishe
3. Mapishi kwa vitendo

KATA-  MWANGATA MTAA - MWANGATA 'A"SIKU YA AFYA NA LISHE YA MTAA:Huduma zilizotolewa ni - Elimu kutoka kwa wataalamu wa ...
10/09/2026

KATA- MWANGATA
MTAA - MWANGATA 'A"

SIKU YA AFYA NA LISHE YA MTAA:

Huduma zilizotolewa ni - Elimu kutoka kwa wataalamu wa kata, Upimaji wa hali ya lishe, Upimaji wa magonjwa yasiyo ya kuambukizwa pamoja na Mapishi kwa vitendo.

SOS CHILDREN VILLLAGES YATOA MAFUNZO YA MASUALA YA UZAZI KWA VIJANA ZAIDI YA 100 HALMASHAURI YA WILAYA YA MUFINDI KUPITI...
10/09/2026

SOS CHILDREN VILLLAGES YATOA MAFUNZO YA MASUALA YA UZAZI KWA VIJANA ZAIDI YA 100 HALMASHAURI YA WILAYA YA MUFINDI KUPITIA MRADI WA (IEA)

Shirika lisilo la kiserikali la SOS Children Villages mkoa wa Iringa limetoa mafunzo
kwa waelimishaji rika wapatao 100 katika Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi ikiwa na lengo ka kupunguza mimba za utotoni.

Akizungumza katika mafunzo hayo yaliyokwenda kwa siku mbili Afisa Mradi katika masuala ya afya ya uzazi na stadi za maisha Jesca Kawonga amesema mafunzo ya waelimishaji rika yaliyofanyika kwa sasa kwa vijana kutoka katika jamii yamekuja mara baada ya kuwafikia vijana wapatao 20000 kutoka katika shule za sekondari katika Halmashauri tofauti na lengo la kuwafikia waelimishaji rika 100 waliopewa mafunzo ni kuwafikia vijana zaidi ya 500 katika jamii.

Naye Muwezeshaji wa kitaifa wa Afya ya uzazi na stadi za maisha pia Muuguzi Mkuu wa mkoa wa Iringa ameeleza kuwa elimu vijana wanayoipata itawasaidia kupata stadi za maisha na kuwapa stadi za kuweza kuhimili mihemko ya kihisia wanayokuwa nayo pia itawasaidia kujitambua na kuweza kupanga maisha malengo binafsi.

Nao baadhi ya vijana waliopatiwa mafunzo wamesema elimu waliyopata hawakuwahi kupata hapo awali na kukiri watakwenda kuwa waalimu wazuri kwa jamii wanazoishi na kuweka malengo yao binafsi na kupuuza masuala ya kujihusisha na kufanya ngono zembe.

Na Neema Masaba

10/09/2026

MUFINDI:

Kwa Mujibu wa Afisa wa Mradi Jesca Kaonga kutoka SOS amesema tayari mradi umewafikia vijana walio shuleni zaidi ya elfu 20 na sasa wameanza mchakato wa kuwafikia vijana waelimisha rika 100 walioko katika jamii kwa kuwajengea uwezo wa stadi za maisha na afya ya uzazi katika umri wa rika balehe.

Bi Kaonga ameongeza kuwa SOS Children’s Villages Tanzania pamoja na kujenga uwezo awali pia kupitia progeamu pia imeweza kuboresha huduma katika Hospitali ya Mji Mafinga na Kituo cha Afya Ihongole (halmashauri yam ji mafinga), Kituo cha Afya Kasanga na Zahanatiy a Nyororo (Halmashauri ya wilaya Mufindi) ikiwa ni juhudi za kuimarisha huduma rafiki kwa vijana na kuwawezesha kupata elimu sahihi ya afya.

Mwezeshaji wa mafunzo ndugu Moses Tawete amesema , mlengo wa mafunzo umeweka mkazo katika kuwezesha vijana ilu waweze kupata taarifa muhimu kuhusu afya ya uzazi, lishe, pamoja na kinga dhidi ya magonjwa mbalimbali kuputia mradi.

Address

Iringa
255

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Makutano Tv posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share