Julius Tanzania Officia

Julius Tanzania Officia John Pombe Joseph

Karibu kwenye ukurasa wangu mpya wa "Julius Tanzania Official" nia na malengo ya kuwepo ukurasa huu ni kuonyesha kazi mbalimbali zinaofanywa na Serikali yetun pendwa ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Jemedari wetu mpendwa Dkt.

WEMA SEPETU AACHIWA HURU NA JESHI LA POLISI BAADA YA KUKAMATWA TENA.
05/07/2019

WEMA SEPETU AACHIWA HURU NA JESHI LA POLISI BAADA YA KUKAMATWA TENA.

“POLISI WAMUACHIA WEMA SEPETU BAADA YA KUMKAMATA JANA > Msanii huyo wa filamu, amenusurika kulala Mahabusu jana baada ya Kituo Kikuu cha Polisi kumuachia huru kwa dhamana hadi hapo watakapomuhitaji > Wema alikamatwa tena jana baada ya Mahakama ya Kisutu kumwachia huru ”

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza kuwa tarehe 31 Julai, 2019 ni siku ya kufanyika uchaguzi mdogo Jimbo la Singi...
05/07/2019

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza kuwa tarehe 31 Julai, 2019 ni siku ya kufanyika uchaguzi mdogo Jimbo la Singida Mashariki lililokuwa likishikiliwa na Tundu Lissu baada ya Spika Job Ndugai kutangaza kuwa jimbo hilo liko wazi.

Ujenzi wa Barabara kutoka mkoani Katavi wilayani Mpanda-Inyonga-sikonge-Tabora kwa kiwango cha lami washika kasi KM 364 ...
02/07/2019

Ujenzi wa Barabara kutoka mkoani Katavi wilayani Mpanda-Inyonga-sikonge-Tabora kwa kiwango cha lami washika kasi KM 364 zaidi ya Billion 300 kutumika.Hongera Dkt Magufuli Rais wa wanyonge, kukamilika kwa Barabara hii kutaifungua Katavi na kuendelea kuwa kinara kwa kilimo .Tukutane site ,Tukutane Kazini.

Utenguzi wa DED - KYELA, MBEYA
01/07/2019

Utenguzi wa DED - KYELA, MBEYA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishuka kwenye ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania A...
01/07/2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishuka kwenye ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania Air Tanzania mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Chato mkoani Geita.

UTEKELEZAJI MATUMIZI BANDARI KAVU KWALA WAANZA!Utekelezaji wa agizo la Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eng. I...
30/06/2019

UTEKELEZAJI MATUMIZI BANDARI KAVU KWALA WAANZA!

Utekelezaji wa agizo la Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eng. Isack Kamwelwe la kuwataka TPA na Wadau wote kuanza mara moja kutumia Bandari Kavu ya Kwala iliyopo Ruvu Mkoa wa Pwani umeanza kwa Wadau kugawana majukumu ya utekelezaji.

Hivi karibuni Waziri Kamwelwe aliunda Kamati maalumu ambayo ameipa jukumu la kuhakikisha Wadau wote wa Bandari ya Dar Es Salaam wanashirikiana na kuanza kutumia Bandari Kavu ya Kwala kufikia mwezi Julai.

Wadau hao wamekutana Julai 29 na kufanya kikao katika eneo la ujenzi wa mradi ambapo wamegawana majukumu ya kuhakikisha kila Mdau anawezesha eneo la mradi ili huduma zianze kutolewa.

Bandari hiyo ya Kwala inatarajiwa kuanza kuhudumia mzigo wa Kontena zinazosafirishwa kupitia Bandari ya Dar Es Salaam ambapo zikifika katika bandari hiyo zitasafirishwa kwa njia ya deli mpaka katika bandari hiyo na baadae kwenda katika mataifa mbalimbali.

Baadhi ya Wadau ambao wamekutana na kupatiwa maagizo ya kuanza utekelezaji ni pamoja na TPA yenyewe, Tanesco, TASAC, TAFAA, TASAA, TANROAD, Suma JKT, TRA, TATOA, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Pwani, Mamlaka ya Maji, Vyombo vya Ulinzi vya Serikali.

Katika picha ni matukio mbalimbali kuhusiana na Kikao cha Kamati hiyo.

 . .
29/06/2019

.

.

DUGAI ATANGAZA KUTENGUA UBUNGE WA TUNDU LISSU: Spika wa Bunge, Job Ndugai, amelitangaza Jimbo la Singida Mashariki kuwa ...
28/06/2019

DUGAI ATANGAZA KUTENGUA UBUNGE WA TUNDU LISSU: Spika wa Bunge, Job Ndugai, amelitangaza Jimbo la Singida Mashariki kuwa wazi baada ya kutengua nafasi ya mbunge wa Jimbo hilo Tundu Lissu kutokana na kile alichokieleza kuwa ni kutotoa taarifa yoyote kwa ofisi ya Spika mahali alipo na kutojaza fomu ya maadili inayotakiwa kujazwa na kila mbunge.

Spika Ndugai amesema tayari amewasiliana na ofisi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi ili kuendelea na mchakato wa kuandaa uchaguzi mdogo wa jimbo hilo.

MTANDAO WA WIZI WA VYUMA VYA KINGO ZA BARABARANI TABORA WANASWAJeshi la Polisi mkoani Tabora limewakamata watu watano wa...
26/06/2019

MTANDAO WA WIZI WA VYUMA VYA KINGO ZA BARABARANI TABORA WANASWA

Jeshi la Polisi mkoani Tabora limewakamata watu watano wanaotuhumiwa kuendesha mtandao wa wizi wa vyuma vya kingo za barabarani.

RPC wa Tabora, ACP Emmanuel Nley amesema polisi iliwakamata watuhumiwa hao wakiwa tayari na vyuma hivyo walivyovifungua katika barabara za Nzega - Tabora na Nyahua - Tabora.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufu...
26/06/2019

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli ameongoza vikao viwili vya Ccm,ambapo awali aliongoza kikao cha Maadili na Usalama na kufuatiwa na kikao cha Kamati kuu ya Chama hicho katika ofisi ndogo za Makao makuu ya Chama hicho Lumumba Jijini Dar es salaam. June 26, 2019

24/06/2019

  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 24 Juni, 2019 amefanya ziara ya kushtukiz...
24/06/2019

wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 24 Juni, 2019 amefanya ziara ya kushtukiza katika mradi wa ujenzi wa daraja linalokatiza baharini kwa kuunganisha maeneo ya Aga Khan na Coco Beach Jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujionea maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo.
Mhe. Rais Magufuli ameshuhudia shughuli za ujenzi zikiendelea vizuri ambapo mkandarasi ambaye ni kampuni ya GS Engineering ya Korea anakamilisha kuunganisha daraja la muda litakalomwezesha kuanza ujenzi wa nguzo za daraja. Kwa ujumla kazi imefikia asilimia 10.12.
Akiwa katika mradi huo Mhe. Rais Magufuli amekutana na Mhandisi Mshauri kutoka kampuni ya Yooshin Engineering Mhandisi Suk-Joo Lee na kumuelezea kufurahishwa kwake na maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo ambalo linatarajiwa kusaidia kupunguza msongamano wa magari kutoka na kuingia katikati ya Jiji la Dar es Salaam.
Nae Bw. Suk-Joo Lee ameelezea kufurahishwa kwake kufanya kazi Tanzania na ameahidi kuwa kazi hiyo itakwenda vizuri.
Daraja hilo litakuwa na urefu wa kilometa 1.03 na barabara za kuunganisha zenye urefu wa kilometa 6.23. Ujenzi wake unahusisha ujenzi wa nguzo za msingi zenye urefu wa kati ya meta 14 na 65 na utagharimu takribani shilingi Bilioni 255.
Daraja hilo limependekezwa kuitwa Tanzanite Bridge na litakamilika Oktoba 2021.

Address

Dodoma

Telephone

+255758376623

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Julius Tanzania Officia posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Establishment

Send a message to Julius Tanzania Officia:

Share

Category