16/05/2017
UNACHOTAKIWA KUJUA KUHUSU UGONJWA WA KISUKARI.(part 1)
Kisukari ni ugonjwa mmoja wapo kati ya magonjwa yasiyo ya kuambukizwa.ugonjwa huu humfanya mtu kuwa na kiwango kikubwa cha sukari yaani glucose kwenye damu.
Ugonjwa huu huibuka mwilini kutokana na hitilafu mbili zinazoweza kujitokeza mwilini k**a ifutavyo'
1.kongosho kushindwa kuzalisha hormone inayo itwa insulini ambayo kazi yake kubwa ni kusaidia chembechembe ndogo za mwili(cell) kutumia chakula/sukari iliyopo kwenye damu kwa ajili ya shughuli mbalimbali za mwili.upungufu wa hormone hii husababisha sukari irundamane kwenye damu.hali hii kitaalam huitwa insulin deficiency.
2.chembechembe za mwili kupoteza uwezo wa kutumia chakula/sukari iliyo katika damu kwa ajili ya shughuli za mwili na kufanya sukari ibakie nyingi kwenye damu ili hali kongosho linafanya kazi yake vizuri.hali hii kitaalamu huitwa insulini resistance.
Dalili za ugonjwa wa kisukari'
1.kujisikia kiu sana kuliko kawaida yako hali ambayo hupelekea kunywa maji mara kwa mara isivyo kawaida
2.kujisikia njaa mara kwa mara,hamu ya kula kuongezeka na kusababisha mtu kula kula muda mwingi
3.kukojoa mara kwa mara hasa wakati wa usiku
Athari za ugonjwa wa kisukari'
Ugonjwa huu ukikaa muda mrefu bila kushusha kiwango cha sukari mwilini huleta athari kubwa sana ikiwemo'
1.magonjwa ya moyo(cardiovascular diseases)
2.magonjwa ya figo(diabetic nephropathy)
3.kiharusi(stroke)
4.upofu wa macho(diabetic retinopathy)
5.vidonda visivyo pona ambavyo hupelekea mtu kukatwa viungo hasa miguu(diabetic foot)