04/03/2021
MAGUFULI K**A NEBUKADNEZA MKUU WA DOLA YA BABELI
“BWANA ASIPOULINDA MJI YEYE AKASHEYE AFANAYA KAZI BURE”
Mwaka 2015 niliandika habari iliyochapishwa na Gazeti TAZAMA “Magufuli k**a Nebukadneza mkuu wa dola ya Babeli” nairudia tena baada ya kusoma Gazeti la RAIA MWEMA “sababu zilizowafanya mitume 11 wasimfuate Yesu majini” mwandishi amemshambulia sana Rais Magufuli.
Mwandishi anadai mwaka 2015 walipopiga kura kumchagua Rais, hawakutarajia Magufuli awe Askofu wa Tanzania, hawakufanya mabadiliko ili Magufuli awe Mwinjilisti mkazi wa Ikulu, Paroko wa kigango cha Magogoni. Hawakutarajia Magufuli awe Mhubiri mwenye upako uliopitiliza mwenye cheo cha unabii na utume wa Kiraisi! Mwinjilisti mfawidhi mwenye kupigiwa saluti.
Madai yote hayo kwasababu tu Rais Magufuli anasisitizia Watanzania kumtanguliza Mungu, hivi karibuni amewataka tena Watanzania kufunga kwa siku tatu ili kumsihi Mungu ainusuru Tanzania na “corona” ndipo mwandishi anapomwona Magufuli anajigeuza Askofu, Shehe, Mchungaji, Nabii na Mwinjilisti. Sijui mwandishi huyo anauchukuliaje uamuzi wa Kanisa Katoliki kumtangaza Nyerere mtakatifu wakati Nyerere hakuwahi kuwa Askofu wala kuwa Kardinali? Mwandishi amewanyamazia Watanzania wanaoihubiri “corona” kwa nguvu k**a kwamba “corona” ndio ugonjwa pekee unaoua!
Hao wote wanaopiga debe la “corona” siyo madaktari waliowatibu marehemu, siyo wasemaji wa familia za waliofiwa wala siyo wasemaji wa Taasisi ambazo marehemu walifanya nazo kazi, isipokuwa wapiga debe la “corona” wamejipa jukumu la kuikampenia “COVID 19 ” wanatumia umaarufu wa marehemu kuitangaza “corona” kibiashara, wanainadai imerudi kwa kasi mpya na nguvu mpya.
Wapiga debe la corona hawatofautiani na waliohamasisha mauaji ya kimbari nchini Rwanda mwaka 1994 waliotumia vyombo vya habari kuchochea mauaji, tofauti ni ndogo kwamba wahubiri wa “corona” wanahamasisha uuaji wa kisaikolojia na kiroho.
Mahubiri yao hasi yatawaacha Watanzania wengi wakiwa hai kimwili lakini ndani wakiwa wafu kiimani, walioaminishwa kwamba (i) “corona” iliyo duniani haishughulikiwi mbingunini
(ii) “corona” iliyotoka nje ya Afrika haisikii dawa yoyote iliyo ndani ya nchi
(iiii) “corona” haitibiki kwa njia za kiafrika isipokuwa tiba zitokazo nje.
(iv) Wapiga debe wanaamini ugonjwa uliotoka nje, unaomuua hata mzungu suluhisho lake haliwezi kupatikana Tanzania, wanaamini corona iliyotoka nje lazima suluhisho lake litoke nje.
Mahubiri yao yameambatana na lawama wanamlaumu Rais Magufuli kwasababu amekuwa jasiri! Wanatamani angesalimu amri awatangazie “superiors” wao walioko nje kwamba Tanzania nayo inakiri kwamba imeshindwa ili walitumie tangazo la kushindwa k**a sumaku ya kuvutia misaada.
Mwandishi anawasoma wapiga debe waliojiinua juu ya madaktari, waliowafunika wataalamu wa Afya na wanaoingilia hadi familia za marehemu wakijigeuza wasemaji wao. Mwandishi haioni jinai yao bali anaona dosari ya Magufuli hadi anamfananisha na Mtume Petro aliyethubutu kutembea juu ya bahari lakini mitume wengine 11 hawakumfuata.
Huyo ambaye leo tunamwita nabii zamani Waisraeli walimwita mwonaji, baadaye wakamwita anayesema kabla hayajatokea, wengine wakamwita mtabiri. Magufuli hasemi mambo kabla hayajatimia, mtu aliyetimiza sifa ya kusema mambo kabla hayajatokea na baadaye yakatokea ni Julius Nyerere, alisema mapema wataibuka watakaowatetea wanyonyaji bila aibu, hayo yametimia “Advocates” wa “imperialism” waliibukia Bungeni, wakaacha kumbukumbu za kudumu kwenye “Hansard” zinazoonyesha utetezi wao. SASA tusubiri kutimia alilosema Nyerere kwamba ataibuka Rais kwa ulevi atajitangaza Rais wa maisha.
Rais Magufuli siyo Askofu, siyo Mwinjilisti, siyo Shehe, siyo mchungaji, siyo Paroko wala siyo Nabii bali ni zaidi ya Nabii, zaidi ya Askofu, Shehe, Mwinjilisti, Paroko na zaidi ya Mchungaji. Kwasababu ameinuliwa na Mungu kwa wakati wake ili afanye wasiyofanya Maaskofu na Mashehe na Wachungaji na Wainjilisti, Magufuli anamtumikia Mungu kwenye nafasi yake ya Urais.
Neno la Mungu linasema msh*taki wa wenye haki Ibilisi ni k**a Simba angurumaye akitafuta mtu ammeze, Shetani amefananishwa na simba aliyezeeka asiyeweza kumrukia mnyama uso kwa uso, bali hujificha mahali akaunguruma kuwatisha wanyama watakaokimbia sauti yake wakakutane na simba wanaok**ata.
David Camerun aliyekuwa Waziri mkuu wa Uingereza aliunguruma kwenye Jumuia ya madola akizitaka nchi za Afrika zibadilishe katiba zao ili zitambue ndoa za jinsia moja, Rais wa Marekani Barack Obama na Cameruni , walitishia kwamba nchi isiyobadilisha katiba yaani isiyoukubali ushoga, isitarajie kupokea msaada wowote kutoka Jumuia ya Ulaya wala Marekani. Tanzania kwakuwa ilitaka kuendelea kupata fedha za bure ilitikiswa, ikaanzisha mchakato wa katiba mpya.
Hao wababe walipounguruma kwa niaba ya Ibilisi hakuna Askofu, Mchungaji, Shehe, Nabii, Mtume wala Mwinjilisti aliyesimama na kweli ya Mungu kuwaambia hapana! Ni Robert Mugabe tu Rais wa Zimbabwe aliyekuwa jasiri kumwambia Obama “ukija Zimbabwe kuhamasisha ushoga itabidi kwanza mimi nikuoe ili tuonyeshe mfano.”
Lakini wengine wote hata wanaojiita wainjilisti wakubwa wa kimataifa, hakuna aliyethubutu kuupinga ufisadi huo ili kuinusuru Afrika. Pope alinyamaza kimya hakuthubutu kuwapigania wakatoliki walioko Afrika, ikumbukwe Yesu alisema “atakaporudi tena mwana wa Adamu, ataikuta imani duniani?” Yesu alimaanisha ataikuta imani ile ile aliyoasisi? Papa hadi leo kwenye suala la ushoga anajigongagonga hayuko uwazi kukiri k**a alivyofundisha Yesu kwamba “ndiyo yenu iwe ndiyo na siyo yenu iwe siyo” lolote lisiloangukia kwenye ndiyo wala hapana linatoka kwa yule MwoVU.
Kwanini namfananisha magufuli na nebukadneza? Kwasababu Mwenyezi Mungu huwainua watu ili kutimiza makusudi yake. Ikiwa amemuinua Magufuli kuwafikishia ujumbe walimwengu, Waafrika na Watanzania, hakuna mwenye ubavu wa kuzuia wala kumwambia Mungu huyo ni Rais wetu, tulimchagua wenyewe kwa kura zetu, hawezi kutumika k**a chombo chako Mungu wakati Mashehe na Maaskofu wapo!
Mungu aliwahi kumtumia Punda kusema k**a mwanadamu, kwasababu Nabii Baalamu alipata wazimu alipolipwa kiasi kikubwa cha fedha ili afanye waliyotaka wanadamu kuacha aliyoyataka Mungu. Hata leo dini “zikibiasharaishwa” (commercialized) viongozi wake wanapagawishwa na nguvu ya fedha hadi wanapoteza mamlaka ya kiroho “moral authority.”
Mfano hai Askofu mkuu wa dhehebu la Anglican alijitangaza kuwa shoga, hakuna Mchungaji wala muumini wa Afrika aliyethubutu kujitenga na Anglikani ya Ulaya wala Marekani, kuashiria kuuchukia uchafu huo! Hakuna mwenye jeuri ya kujitenga azikose dola za Marekani na Euro za Ulaya! Hawa ndio watakaofungisha ndoa za jinsia moja kwenye madhehebu yao, ni mtihani mgumu kati ya kuikiri nguvu ya Yesu kwa kushik**ana naye ama kuikiri nguvu ya fedha na kumkana Yesu. Fedha ndio ilimfanya Nabii Baalamu apate wazimu hadi akasababisha Punda kusema k**a binaadamu.
Mwenyezi Mungu hafungwi na mifumo ya dini na madhehebu, wala kwenye mapambano ya ukombozi Mungu hawekewi mipaka na wanadamu. Wapigania uhuru walioongoza TANU walimhusisha Mungu kwenye mapambano yao, mashehe walimshurutisha Julius Nyerere kufunga pamoja nao ingawaje walimfahamu hakuwa mwislamu.
Wakati wa mapambano Nyerere aliwahi kuulizwa swali ingekuwaje endapo Mwingereza angegoma kutoa uhuru? Waliomuuliza walitarajia Nyerere ajibu k**a kiongozi mwoga ama ajibu kishujaa ili nao Watanganyika wachukue msimamo k**a wa Kenya ambako Mzee Jommo Kenyata alikuwa amewaingiza wananchi kwenye mapambano ya umwagaji damu, waliyaita MAUMAU yaani Mzungu Arudi Ulaya Mwafrika Apate Uhuru.
Nyerere alijibu kwa utulivu kwamba Gavana akigoma kutoka, tutamsh*takia Malkia, asipotusikiliza Malkia tutash*taki Umoja wa Mataifa, huo usipotusikiliza tutamsh*takia Mungu. Huo ni uthibitisho kwamb a tangu awali Watanganyika walimtanguliza Mungu, walimwamini na kumkiri kwa kila gumu walilokutana nalo maishani mwao, ndio maana uhuru ulipopatikana waasisi walikumbuka kumtaja Mungu na kumkiri kwenye wimbo wetu wa Taifa.
Tunapoimba “Mungu ibariki Afrika, uwabariki viongozi wake, uwape hekima, kwakuwa hekima na umoja ndio ngao zetu ama kinga yetu sisi Afrika na watu wake” dua hili halielekezwi kwa Jabali wala sanamu la kuchongwa lisilosikia, lisilojibu wala lisiloweza kufanya lolote, bali tunamwomba Mungu aliye hai.
Watanzania tunapoimba “Mungu ibariki Tanzania, dumisha uhuru na umoja kwa wote, wanawake, wanaume na watoto” hatuombi kwa HAKUNA, isiyoyosikia, isiyoitika wala isiyotenda. Tunamwomba yeye ambaye yuko, mwaminifu na wa haki, hao waliotetereka kiimani yaani wanaoamini kwamba maendeleo ya sayansi na tekinolojia yatakuwa mbadala wa Mungu wasitulazimishe kuikubali hiyo imani yao iliyokengeuka, imani iliyompindua Mungu duniani, ikamgeuza awe Mungu wa mbinguni tu.
SISI wengine bado tunaamini
(i) Mungu anatakiwa kutawala dunia 100%.
(ii) Mungu k**a alivyo Mungu huko Mbinguni ndivyo alivyo Mungu hapa duniani
(iii) Mungu k**a anavyohusika na mbinguni ndivyo anavyohusika pia na dunia yetu kwa kiasi kile kile anachohusika mbinguni.
(iv) Mungu ni yule yule wa zamani wa sasa na baadaye
Mtu anayejiona amesoma, ameelimika, ameendelea na amepiga hatua kisayansi na kitekinolojia na kwahiyo awe amepevuka kiasi kwamba upevu wake unamtosha, unamfanya asimtegemee tena Mungu maishani mwake, huyo tumwambie wazi uasi wake asiuingiza kwenye dola. KWASABABU dola ni yetu wote tunaoamini na wasioamini, Rais Magufuli ni wetu wote, wasitokee wanaolazimisha Rais wa Tanzania awe mali ya wasioamini tu.
Tanzania ni dola iliyoanza na Mungu tangu ikiitwa Tanganyika, imeendelea na Mungu hadi leo na itaendelea na Mungu hadi kiama, wanaweza kuibuka viongozi wakengeufu lakini bado hatakosekana Mtanzania japo mmoja wa kusimama kwa niaba ya Mungu.
Mwenyezi Mungu kwa kinywa cha Nabii Yeremia anamwita Nebukadneza mtumishi wangu, Nabii Yeremia amelirudia neno hilo “mtumishi wangu Nebukadneza” mara sita. Wakati Nabii Yeremia akimtaja Nebukadneza Mfalme wa Babeli k**a mtumishi wa Mungu, huyo Nebukadneza mwenyewe hakuwa akimjua Mungu wa Waisraeli. Nebukadneza alikuwa na miungu yake ya kibabeli. Kumbe ilikuwaje Mungu asimwite mtumishi wangu Mfalme Sedekia wa dola ya kidini ya Israeli, bali amwite Nebukadneza ambaye kulingana na dini ya wayahudi aliitwa “kafiri?”
Kwanini Mungu hakuwaita Makuhani na viongozi wa dini ya kiyahudi watumishi wake bali akamwita Nebuukadneza ambaye leo kwa viwango vya madhehebu yaliyotoka Ulaya ni “pagano” ama “gentile?” Hapa ndipo unatakiwa uelewa kwamba Mungu hafugwi kwenye taratibu za wanadamu, Nebukadneza aliitwa mtumishi wa Mungu kwasababu aliitwa kulitumikia shauri la Mungu.
Nebukadneza aliitwa mtumishi wa Mungu kwasababu kwa nafasi yake k**a Mfalme aliutimiza mpango wa Mungu, inabidi tukubali kwamba kuna mambo hapa duniani ambayo Mungu hawezi kuwatuma Malaika kuyafanya ili malengo (mapenzi) yake yatimizwe, bali atawatumia wanadamu kwa nafasi zao ama kwa kaliba zao.