Kyaro cul breeze Pub n Pool.

Kyaro cul breeze Pub n Pool. Kyaro cul breeze pub locate at Diwani street Chang'ombe former Railway quaters in Temeke district Da

Sound system for hiring in different events at a reasonable price. Inbox for more detail.
15/11/2025

Sound system for hiring in different events at a reasonable price. Inbox for more detail.

11/09/2024

Konda anauliza KWASADALA hamna zaidi ya mara 3 nikajikuta namwambia BOMANG'OMBE shusha!! Kumbe niko Kigamboni...

22/04/2024

Chagua bega, Donda la maana,Tua tugawe,Kamba,Mdani,Mpe bapa,Kwala,Sunda,Minya,chochora....
UNAKUMBUKA MISAMIATI GANI YA KITAANI?

Kwa niaba ya uongozi wa Kyaro cul breeze Pub n Pool. NAWATAKIA NYOTE HERI YA 2023.
16/01/2023

Kwa niaba ya uongozi wa Kyaro cul breeze Pub n Pool. NAWATAKIA NYOTE HERI YA 2023.

06/04/2022
26/08/2018

Enjoy ya drink,while sitting at our place.

LEO KATIKA HISTORIA YA TANZANIA:  MJUWE MZEE JUMBE MUHAMMAD TAMBAZA NI NANI ❓Mzee Jumbe Muhammad Tambaza, alizaliwa Janu...
30/07/2018

LEO KATIKA HISTORIA YA TANZANIA:
MJUWE MZEE JUMBE MUHAMMAD TAMBAZA NI NANI ❓

Mzee Jumbe Muhammad Tambaza, alizaliwa January 1891 ni mmoja katika wapigania uhuru mashuhuri wa nchi hii ambao, historia inawataja k**a ni watu waliotoa mchango mkubwa sana katika kufanikisha kumng’oa Mkoloni Mwingereza, katika ardhi yetu tukufu.

Hayati Mzee Tambaza, ambaye alifariki mnamo July 21, 1978. Ikiwa ni miaka 40 tangu kifo chake , anaingizwa katika kundi moja la watu wa mwanzo kabisa waliompokea kwa furaha na upendo kijana Julius Nyerere kutoka Butiama, alipofika jijini Dar es Salaam kwa kumuunga mkono ‘mia kwa mia’, katika harakati zake za kupigania uhuru wa Tanganyika kwenye miaka ya 1950s.

Wanaharakati wengine aliokuwa nao ni pamoja na Mzee Mwinjuma Mwinyikambi wa Mwananyamala; Mzee John Rupia wa Mission Quarters; Sheikh Suleiman Takadir; Sheikh Haidar Mwinyimvua (Kisutu); Mzee Max Mbwana (Kariakoo); Zubeir Mwinshehe Mtemvu (Gerezani) pamoja na familia ya Mzee Azizi Ali (Mtoni) na ile ya Kleist Sykes (Gerezani), Dar es Salaam.

Ukoo wa Diwan Tambaza Zarara bin Mwinyi ndio waliokuwa wenyeji wa maeneo ya katikati ya jiji wakati huo, wakihodhi eneo la ardhi yote ya Upanga, iliyosambaa kuanzia Daraja la Selender kuelekea Palm Beach Hotel, hadi Ikulu ya Magogoni kwa upande mmoja; na kwa upande mwengine maeneo yote kutoka Aga Khan Hospital, Ocean Road Hospital, Kivukoni Front (makaburi ya asili ya wanandugu wengine yako pale Wizara ya Utumishi, Magogoni) kwenda Mnara wa Saa pale Uhuru Street na vilivyomo ndani yake.

Habari zinasema kwamba, katika siku za mwanzo tu za kupambana na Mwingereza, wazee mashuhuri wa hapa Dar es Salaam walikutana na kuamua kumfanyia ‘zindiko’ na ‘tambiko’ la kijadi, pamoja na kumwombea dua maalumu kijana mdogo, Julius Nyerere, ili kumkinga na waovu na pia kuifanya nyota yake ing’are juu ya wote wenye nia mbaya naye; wakiwamo watawala wa Kiingereza, hasa Gavana Twinning.

Katika moja ya hotuba zake za kuaga aliyoitoa mnamo Novemba 5, 1985, Nyerere alilikumbumbuka tukio hilo na hapa chini anasimulia:

“…Mimi nimeanza siasa na wazee wa Dar es Salaam; na wazee wa Tanzania…na mambo makubwa k**a haya k**a hayana baraka za wazee hayaendi… huwa magumu sana. Wanasema ngoma ya watoto haikeshi! Mimi nilipata baraka za wazee tangu zamani; tangu awali kabisa.

“Sasa siku moja, Dosa akanifuata Magomeni (nyumbani kwake) akasema: ‘Leo wazee wanakutaka. Wapi? Kwa Mzee Jumbe Tambaza. Wanakutaka usiku. Nikasema haya, nitakuja. Nikaenda. Nikakuta wazee wameshakaa wameniita kijana wao kuniombea dua. Mimi Mkristo wao Waislamu watupu. Wakaniombea dua za ubani. Tuk**aliza.”

Anahadithia Mwalimu na kuendelea:

“Tulipomaliza wakasema kuna dua pia za wazee wao. Basi wakanitoa nje. Tukatoka. Zilipomalizika… zilikuwa za Korani; sasa zikaja dua za wazee… za jadi, “…walikuwa na beberu la mbuzi… wamechimba shimo. Wakaniambia simama. Nikasimama beberu akachinjwa huku anaambiwa Twinning ‘umekwisha’… nikaambiwa tambuka… nikavuka lile shimo na baada ya hapo nikaambiwa …basi nenda zako kuanzia leo Twinning amekwisha!”

Mwalimu alimaliza kusimulia namna alivyofanyiwa dua na tambiko nyumbani kwa Mzee Tambaza, Upanga jijini.
Kutawaliwa na Wazungu kuliwakera na kuwakasirisha watu wengi sana, kutokana na kule kudharauliwa ndani ya nchi yao wenyewe na watu wengine; hasa pale walipominywa katika kupatiwa huduma muhimu k**a elimu bora, matibabu na mahala pazuri pa kuishi.

Pamoja na mambo mengi mengine yaliyokuwa mabaya kutokana na kutawaliwa, yamo pia na yale ya kuwekwa kwa madaraja katika utoaji huduma muhimu. Sisi, wana wa nchi hii, hatukuwa na shule za maana hata kidogo; watu wote sisi tukasomee shule moja tu (Mchikichini) mpaka darasa la nne; kwa nini hasa k**a siyo dharau?

Nyumba zetu za kukaa zilikuwa za ovyo zilijengwa kwa miti na kukandikwa udongo na juu ni makuti, tena hapa hapa mjini Dar es Salaam, sikwambii vijijini; umeme uko kwenye taa za barabarani na siyo majumbani mwetu. Tukiwasha vibatari na taa za ‘chemli za Aladin’ kwa wenye uwezo kidogo kila siku.

Hospitali ziliishia kutoa k**a huduma fulani ya mwanzo tu (First Aid). Haikuwapo hospitali ya Amana, Temeke, Mnazi Mmoja, Mwananyamala wala Mbagala. Tuliponea kibahatibahati tu kwa mizizi na majani ya porini. Ukiwa na homa kali basi chemsha mwarobaini; tumbo la kuendesha chemsha majani ya mpera au mpapai nani akupe ‘antibiotic wewe’.

Hospitali ya Muhimbili, yenye maabara na vipimo pamoja na madaktari bingwa, ilijengwa mwaka 1957 - ni juzi tu - kwa heshima ya Binti Mfalme Margareth II, aliyekuwa na ziara ya kutembelea makoloni ili aje kufungua rasmi hospitali hiyo. Kiwanja kilitolewa kwa hisani ya familia ya Mzee Jumbe Tambaza, ambapo miembe ile mikubwa inayoonekana mpaka leo pale ilikuwa shambani kwa kina Tambaza.

Kwa hivyo basi, ukiacha labda homa na vidonda, magonjwa mengine yote kwetu ilikuwa ni kifo tu. Umri mkubwa wa kuishi kwa wastani ulikuwa ni miaka 30.

Mzee Jumbe Tambaza, ambaye jina lake linanasibishwa na shule maarufu ya Sekondari ya Tambaza ya jijini - hana uhusiano wowote na shule hiyo - shule ilipewa jina lake kutokana na eneo iliyopo na kwa kuthamini mchango wake katika kupigania uhuru.

Kabla ya hapo, wakati huo wa ubaguzi wa rangi na matabaka, shule hiyo na ile ya msingi iliyo jirani nayo inayoitwa Muhimbili Primary, zilikuwa mahsusi kwa vijana wa Kihindi tu – hasa Ismailia - zikijulikana k**a ‘Aga Khan Schools’ na kamwe hawakuwa wakisoma Waswahili na Kiswahili pale.

Shamba la Mzee Jumbe Tambaza pale Upanga, lilianzia mbele kidogo ilipo Shule ya Jangwani Wasichana (ambayo wakati wa ukoloni ilijengwa na serikali wasome watoto wa k**e wa Kihindi tu, na ile Shule ya Azania ilikuwa kwa watoto wa Kihindi wa kiume), na kutambaa moja kwa moja mpaka lilipo Daraja la Selender pale baharini.

Eneo la Majengo ya Hospitali ya Muhimbili ilikuwa mali ya Jumbe Tambaza na marehemu nduguze (Msakara, Kudura na Mwamtoro Tambaza). Kutokana na kukosekana kwa hospitali ya maana ya rufaa kwa ajili ya Waafrika (kwa sababu ya ubaguzi tu), hayati Mzee Tambaza alitoa eneo lote lile la Muhimbili ijengwe hospitali ya Waafrika ili kupunguza vifo vilivyotokana na kukosa tiba sahihi.

Kijihospitali kidogo kwa ajili ya watu Weusi kilikuwapo pale jirani na Kituo cha Kati cha Polisi (Central Police Station) jijini, ikiitwa Sewa Haji Hospital, kwa heshima ya mfadhili aliyeijenga kusaidia jamii masikini. Sewa Haji alikuwa mkazi wa Bagamoyo mwenye asili ya Kibulushi kutoka Persia. Baada ya kujengwa hospitali yaj Muhimbili, jengo moja katika yale matatu makuu, likaitwa Sewa Haji k**a kumbukumbu yake.

Mjini Dar es Salaam wakati huo wa kibaguzibaguzi, serikali ya kikoloni haikutenga sehemu ya kuzikia watu weusi ambao walikuwa daraja la nne. Yale makaburi mashuhuri ya Kisutu, wakati huo yalikuwa ni ya watu wenye asili ya Kiarabu tu! Mwengine yoyote, ilibidi apelekwe kijijini kwao tu nje ya mji – Kunduchi, Mbweni, Msasani, Bagamoyo, Kisarawe, Maneromango na mikoani pia.

Sasa, ili kuondoa adha hiyo na usumbufu, Babu Mzee Tambaza, alitoa bure sehemu kubwa ya eneo lake itumike kwa watu wenye kuwa na shida ya kuzika ndugu zao jijini. Makaburi ya Tambaza siku hizo yalikuwa maarufu sana kuliko yalivyo yale ya Kisutu kwa sasa. Kamwe watu weusi hawakuwa wakizikwa Kisutu, k**a ilivyo wakati huu.

Kufuatia hali hiyo, Jumbe Tambaza aliwashawishi binamu zake wawili, Mwinyimkuu Mshindo na Diwan Mwinyi Ndugumbi na wao wakatoa sehemu watu waweze kuzikana kule maeneo ya Mwinyimkuu, Magomeni Mapipa na Ndugumbi, Magomeni Makuti; makaburi ambayo mpaka leo yameendelea kutumika kuzikia watu wote.

Neno, ''Tambaza,'' limetokana na neno ''kutambaa,'' au ''kusambaa,'' eneo kubwa. Diwan Tambaza na nduguze walikuwa watawala wa sehemu mbalimbali za hapa Mzizima siku za nyuma kabla Waarabu, Wajerumani wa Wangereza kufika hapa. Nduguze wengine ni Diwan Uweje; Diwan Uzasana; Diwan Mwenye-Kuuchimba na Diwan Mwinyi Ndugumbi.

Majina hayo walijipachika wenyewe kiushindani, kujigamba na kujitukuza kuliko ndugu wengine; hivyo kimafumbo mafumbo, huyu akajiita hivi na yule akamjibu mwenzake vile; mwengine akajiita naye atakavyo, kutokana na uhodari na tawala thabiti walizoziongoza.

Majina hayo pandikizi, hata hivyo yalikuwa na maana yake kila moja; k**a vile mtu aseme mimi ‘Mobutu Sese Seku Kuku Mbenju wa Zabanga’, ikiwa na maana ya ushujaa kwa ‘Batu ba Kongo na fasi ya Zairwaa!’

Sasa Diwan Tambaza alipojiita vile, nduguye Diwan Uweje akamjibu na kumwuliza hata ukiwa umesambaa ndio uweje? Mwengine naye akasema, ‘’Ah! Uliza sana wewe uambiwe.’’ Hivyo yeye akajita Diwan Uzasana. Diwan Mwenye-Kuuchimba, yeye alikuwa akitawala maeneo ya Mtoni Kijichi na Mbagala yake, akasema, ‘’Nyie wote mnacheza tu, ‘mimi ndiye mwenye kuuchimba!’’ Kwa maana ya kwamba ndio kiboko ya wote. Ilimradi hali ikawa ndiyo hiyo; na hizo ndio zama zao, kwani husemwa kila zama na kitabu chake.

Mwandishi wa makala haya, ni mjukuu Mzee Saleh bin Abdallah Tambaza wa Zarara, anakuwa ndugu wa Mzee Jumbe Muhammad Tambaza, yaani baba zao walikuwa ndugu.

Shamba la babu yangu linasambaa kuanzia Don Bosco, Makao Makuu ya Jeshi, Diamond Jubilee, Msikiti Maamur (kaburi la babu na babake babu yamo ndani ya Msikiti wa Maamur unapoingia mkono wa kulia pale ukutani), kuelekea kwenye Jamat la Wahindi mpaka Mahak**ani kule Kisutu.

Miembe, minazi na mizambarau ile ya asili inayoonekana Upanga, ilipandwa na babu yangu kwa ajili ya urithi wa wajukuu zake, itakapofika zamu yao kumiliki maeneo yale.

Kwa bahati mbaya sana, Wazungu Waingereza, wakaona mandhari ile nzuri ya Upanga, hawakustahili watu weusi kuishi pale na wakawaamuru babu zangu wahame wawapishe Wahindi raia daraja pili. Hii ni baada ya wao Wazungu daraja la kwanza kuchukua eneo lote la Oysterbay (sasa Masaki). Maeneo yote hayo mawili yenye upepo mwanana ni karibu kabisa na bahari.

Kitendo cha kumhamisha mtu nyumbani kwake kwa namna ile, halafu kumpa fidia uitakayo wewe, ni dharau, dhuluma na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu. Wazee wale wastaarabu na wajanja hawakuwa na haja ya kuyauza maeneo yale, kwani ukiyaangalia utaona waliyapangilia ili vizazi na vizazi vya kwao viishi hapo.

Hii haihitaji mjadala wala maelezo marefu, lakini ni ushahidi tosha kwamba inaweza ikawa ndiyo sababu kubwa iliyomfanya Mzee Jumbe Tambaza awe mstari wa mbele kabisa katika kuwachukia watawala wa Kizungu na kumuunga mkono Nyerere kwa nguvu kubwa k**a ile.

Mchango wa Mzee Jumbe Tambaza katika ukombozi wa nchi yetu haukutetereka hata kidogo, kwani hata pale rafiki yake mpenzi Sheikh Suleiman Takadir, alipotahadharisha watu kuwa makini na Nyerere maana ameonyesha kwamba siku za usoni angependelea zaidi jamaa zake, Mzee Jumbe hakumuunga mkono na akakubali Sheikh Takadiri atengwe na jamii kwa manufaa ya umoja wa kitaifa.

Jumbe Tambaza pia hakumuunga mkono Zubeir Mtemvu, kwenye suala la Kura Tatu ambalo ilibaki kidogo tu chama cha Tanu kingesambaratika na kuwa vipande viwili; lakini yeye alibaki na Nyerere wake mpaka dakika ya mwisho kule Tabora hadi kukasainiwa waraka wa ‘Uamuzi wa Busara’ ambao uliwapeleka TANU kwenye Uchaguzi wa Kura Tatu.

Katika picha ya pamoja iliyopigwa baada ya kutangazwa ushindi wa kuingia kwenye Kura Tatu kwa chama cha TANU, anayeonekana nyuma ya Mwalimu Nyerere pale Tabora ni Mzee Jumbe Tambaza. (Rejea kitabu Mohammed Said, ‘’Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes… uk 275).

Kutokana na uaminifu wao usiotetereka kwa chama chao, Mzee Jumbe Tambaza na mwenziwe Mzee Mwinjuma Mwinyikambi; wazee wale wawili wa Kimashomvi kutoka Mzizima, kwa muda mrefu wamekuwa wajumbe wa kudumu (permanent seats) kwenye Kamati Kuu ya TANU bila kupigiwa kura; achilia mbali ule uwepo wao kwenye Baraza la Wazee wa TANU.

Mnamo mwanzo wa miaka ya mwanzoni 1950, Mzee Tambaza alitumbukizwa tena kwenye mgogoro mkubwa na serikali pale ilipokuwa inajenga upya Barabara ya Umoja wa Mataifa kutokea Faya kuelekea Daraja la Selander, ilipoamuliwa kwamba sehemu ya eneo la makaburi iondoke kupisha ujenzi huo.

Hayati Mzee Tambaza, alifungua kesi mahak**ani dhidi ya serikali, kesi ambayo inatajwa k**a moja ya kesi nzito (landmark cases) sana kutokea hapa nchini na Afrika Mashariki iliyogusa imani ya Dini ya Kiislamu; kwamba je, ni halali au si halali kufukua makaburi ya watu waliokufa?

Kesi ya Makaburi, k**a ilivyokuja kujulikana, iliunguruma kwa muda mrefu na kujaza kurasa za mbele za magazeti wakati huo, kutokana na mabishano makali ya hoja (cross examinations) mahak**ani baina ya mawakili wa pande mbili hasimu.

Wakati serikali ikiwatumia masheikh wazawa wa hapa waliosema kwamba inakubalika kufukua makaburi, Jumbe Tambaza aliwatumia masheikh wakubwa kutoka Mombasa na Zanzibar, akiwemo aliyekuwa Kadhi wa Zanzibar Abdallah Saleh Farsy kupinga hoja hizo.

Kwa kishindo kikubwa, Mzee Tambaza alishinda kesi ile na ikabidi barabara ile ipindishwe pale kwenye mteremko wa kutokea Faya na kuyaacha makaburi na vilivyo ndani yake k**a yalivyo. Haraka haraka, Hayati Mzee Tambaza akafanya maamuzi ya kujenga msikiti ambao haukuwapo mahala hapo kabla ya tukio hili, kuepusha kujirudia.

Huyo ndiye Mzee Jumbe Muhammad Tambaza, mwanaharakati wa kupigania uhuru wa taifa hili wa kupigiwa mfano, aliyetetea na kutoa vyake kusaidia wanyonge wenziwe katika jamii yetu katika kipindi cha manyanyaso ya utawala dhalimu wa Malkia wa Uingereza. Alimfanyia madua na matambiko ya jadi Mwalimu Nyerere ili nuru yake ing’are k**a mwezi na jua!

Ewe Mola – ilaze roho ya marehemu mahala Pema peponi- Aamin

21/05/2018

Ni jioni nyingine tena ya jumatatu baada ya pilika za mchana kutwa huu ndio wakati wa kupata kutuliza akili kwa vinywaji na jikoni kuna chakula safi kabisa....

Nyote mnakaribishwa.

Good friday
30/03/2018

Good friday

Waziri Mkuu mstaafu wa Israel Ehud Barak na familia yake walikuja nchini kutalii na moja ya maeneo waliyofika ni Oldupai...
20/09/2017

Waziri Mkuu mstaafu wa Israel Ehud Barak na familia yake walikuja nchini kutalii na moja ya maeneo waliyofika ni Oldupai Gorge, sehemu inapopatikana historia muhimu ya binadamu.

Eneo hilo linalotajwa kuwa la ajabu lipo ndani ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, takriban kilomita 150 kutoka Arusha mjini na takriban kilomita 800 kutoka jijini Dar es Salaam.

Baada ya kutembelea eneo hilo, Barak alitoa kauli moja tu: “Hapa ni eneo muhimu sana duniani kwani ndiyo makutano ya historia ya binadamu.”

Barak alikuwa Waziri Mkuu wa Israel mwaka 1999 hadi 2001, akiwa kiongozi wa Chama Labor hadi mwaka 2011 na pia aliwahi kuwa Waziri wa Ulinzi wa Israel kuanzia 2007 hadi 2013.

Wakati Waziri Mkuu huyo wa zamani na familia yake wanafunga safari kuja nchini katika eneo la Oldupai umbali wa takriban kilomita 6,000, Watanzania ambao wanaishi kilomita chini ya 200 tu hawajawahi kufika eneo hili.

Takriban saa tano nimekuwa katika eneo hili nashuhudia idadi kubwa ya watalii kutoka nje ya Tanzania wengi wakiwa na familia zao, wakifika hapa kupata historia ya eneo hili, lakini Watanzania ninao waona ni madereva wa magari yaliyoleta watalii na wafanyakazi wa eneo hili.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Lamo Makani anasema eneo la Oldupai ni eneo muhimu sana katika historia ya mwanadamu.

Makani anasema eneo hili, pamoja na eneo la jirani la Laitole ambalo zipo alama za nyayo zenye zaidi ya miaka milioni 3.6 za zamadamu linapaswa kulinufaisha Taifa.

“Ni ukweli uliowazi kuwa bado hatujalitumia vizuri sana eneo hili kuvuta mamilioni ya watalii duniani na Watanzania, lakini k**a wizara tunaendelea kuhakikisha eneo hilo ambalo Mungu ametujalia linatunufaisha” anasema.



Kuna nini Oldupai?

Mhifadhi wa malikale katika bonde la Oldupai, John Paresso anasema eneo hili ni chimbuko la historia ya zamadamu na kuna ushahidi wa zaidi ya miaka milioni mbili iliyopita.

Anasema jina halisi la eneo hilo ni Oldupai na siyo Olduvai k**a ambavyo lilielezwa na mmoja wa watafiti wa mwanzo wa eneo hili, Profesa Wilhalm Katt Windle ambaye alishindwa kutamka vyema neno la Kimasai Oldupai na kusema Olduvai.

Paresso anasema Oldupai ni jina la kimasai ambalo lina maana ya katani ambazo zinapatikana katika bonde hilo.

Katani hizo ni nyembamba tofauti na katani za kawaida na zinahimili hali ya joto na ukame katika eneo hilo.

Anasema katika bonde hili, kuna mabaki mbalimbali za damadamu wa kale na wanyama ambao hivi sasa hawapo tena duniani ambao waliishi zaidi ya miaka milioni mbili iliyopita.

Miongoni mwa wanyama hao ni tembo wa kale, nyati wa kale ambao walikuwa na pembe ndefu zaidi ya ng’ombe, farasi wa kale, swala na twiga wa kale ambao walikuwa na pembe ndefu.

Katika eneo hili pia kuna mabaki mbalimbali ya zamadamu walioishi miaka zaidi ya millioni mbili iliyopita, kuna mawe ambayo yalitumika kwa shughuli zao mbalimbali na zana nyingine.

Katika bonde hili pia kuna matabaka sita ya udogo na tafiti zimefanyika kuanzia miaka milioni mbili iliyopita hadi miaka 100 iliyopita.

Anasema tafiti nyingi ambazo zinaendelea katika bonde hilo zinafanywa katika matabaka hayo sita na imegundulika kuna mabaki ya zamadamu wa kale, visukuku na wanyama mbalimbali wa kale.

Katika matabaka hayo, takala la sita lenye miaka zaidi ya milioni mbili iliyopita, yaliguliwa mabaki ya zamadamu wa kale (Australepithe cus boisei).

Tabaka la pili lenye umri wa zaidi ya miaka milioni 1.9 yalipatikana mabaki ya zamadamu aliyekuwa anatumia mikono (Homo habilis na Zinjanthoopus).

Paresso anasema tabaka la tatu yalipatikana mabaki ya zamadamu (Homoerectus) ambaye alikuwa anatembea miaka kati ya milioni 1.5 hadi 500,000.

Anasema watafiti katika tabaka la nne ambalo lina miaka kati ya 400,000 hadi 200,000 iliyopita walikuta mabaki ya zamadamu Homo Ectus ambaye alikuwa anatumia mikono, sawa na tabaka la miaka 100,000 hadi 10,000 iliyopita.

“Katika maeneo haya pia kuna mabaki ya wanyama wa kale ambao wengi hawapo hivi sasa hali ambayo inaonyesha umuhimu wake,” anasema.

Mhifadhi Msaidizi katika Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Orgoo Mauyai anasema utajiri wa historia katika eneo la bonde la Oldupai ni mkubwa na bado utafiti unaendelea.

“Hadi sasa bado kuna watafiti wanaendelea kugundua vitu mbalimbali katika bonde hili hadi maeneo la Laetoli na tunaimani mengi yatagundulika na hivyo kuvutia mamilioni ya watalii,”anasema.



Ugunduzi unaoendelea

Licha ya utafiti katika bonde hili ulioanza tangu mwaka 1913 uliofanywa na Wajerumani na baadaye utafiti wa Dk louis Leakey na mkewe Mary, waliopata visukuku 60 vya zamadamu bado hadi sasa utafiti unaendelea na umekuwa na mafanikio makubwa.

Hivi karibuni watafiti wa mambo ya kale na wanasayansi kutoka mataifa ya Ulaya, Amerika na Afrika, wamegundua masalia 19 zaidi ya visukuku vya zamadamu katika eneo la hifadhi ya Ngorongoro na hivyo kuanza kuamini kuwa bustani ya Edeni ilikuwa Ukanda wa bonde la Ufa wa Ngorongoro, Kenya na Ethiopia.

Vitabu vitakatifu vinaitajwa bustani ya Eden kuwa ni eneo ambalo binadamu wa kwanza Adamu na Eva (Hawa) waliishi kabla ya Mungu kuwatoa baada ya kumuasi.

Profesa Phidelis Masao wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Idara ya Mambo ya Kale anasema katika eneo la bonde la Oldupai Gorge, watafiti hao, walipata masalia hayo ya visukuku vya zamadamu 19 yanafanya eneo la Ngorongoro pekee kupatikana masalia 79.

Profesa Masao anasema ugunduzi mpya unaoendelea katika eneo la Oldupai na Laetoli unathibitisha huenda binaadamu wa kwanza waliishi katika mabonde hayo.

“Ugunduzi huo, sambamba na unaoendelea katika maeneo ya Turkana nchini Kenya na Afaa nchini Ethiopia unaonyesha kuwa eneo la bonde la ufa kutoka Tanzania, Kenya na Ethiopia ndiyo ilikuwa bustani ya Edeni,” Profesa Masao.

Naye, Profesa Robert Blumeuschine kutoka taasisi ya utafiti wa mambo ya kale ya Past ya nchini Afrika ya kusini anasema eneo la Ngorongoro ni muhimu kwa sasa kwa historia ya dunia.

Profesa Blumeuschine anasema watafiti wote wakubwa duniani wataendelea kufika Ngorongoro ili kujua vitu vingi kuhusiana na historia ya mwanadamu.

Katika eneo hilo la Laetoli karibuni pia yamegundulika mabaki ya zamadamu wanadaiwa kuishi miaka milioni 3.7 iliyopita.

Ugunduzi huu ni wa pili mkubwa kufanyika baada ya ule wa Dk Mary Leaky na wenzake uliofanywa mwaka 1978 katika eneo hilo.



Mikakati ya boresha Oldupai

Kutokana na umuhimu wa eneo hili la Oldupai na mengine ambayo sasa yanatambulika k**a maene ya utalii wa kijiolojia (Geopark), Jumuiya ya Ulaya (EU) tayari imetoa kiasi cha Sh4.2 bilioni kuboresha maeneo haya.

Meneja wa Idara ya Urithi wa Utamaduni wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Mhandisi Joseph Mwankunde anasema fedha hizo, zimetolewa kuboresha mradi wa maeneo muhimu kijiorojia katika hifadhi hiyo ambayo ni urithi wa utamaduni na vivutio cha watalii.

Anasema fedha hizo zitatumika katika uboreshaji na ujenzi wa jengo la makumbusho la oldupai, majengo ya kuuzwa bidhaa za asili, njia za kutembelea watalii katika eneo la ziwa Natron, mazingira ya Mlima Oldonyolengai na maeneo ya Creta ya Ngorongoro na Laitole.

Mhifadhi Mkuu wa Ngorongoro, Dk Fred Manongi anasema mamlaka hiyo imejipanga kuongeza idadi ya watalii katika hifadhi hiyo kupitia Bonde la Oldupai na maeneo mengine ya vivutio.

Anasema kwa sasa watalii wanaotembelea hifadhi ni kati ya 700,000 hadi 800,000 kwa mwaka idadi ambayo ni ndogo kulinganisha na watalii wanaopaswa kuja nchini hasa kutokana na vivutio muhimu vilivyopo Ngorongoro.

“Tunataka kuendeleza eneo hilo la utalii ya kijilojia kwani ndiyo utalii mpya ambao unapendwa na nchi za Asia k**a China na tunatarajia kuongeza watalii wa ndani na nje kuja Oldupai na maeneo mengine kuona urithi hii,” anasema

Night hourz @
18/08/2017

Night hourz @

Utafiti umebainisha kwamba kufanya mapenzi angalau mara tatu kwa wiki kunapunguza uwezekano wa kupatwa Heart Attack (Sha...
16/08/2017

Utafiti umebainisha kwamba kufanya mapenzi angalau mara tatu kwa wiki kunapunguza uwezekano wa kupatwa Heart Attack (Shambulio la Moyo) kwa 50% ukilinganishwa na yule ambaye anapitisha wiki nzima bila kupiga mambo yetu. Pia utafiti huo unasisitiza ya kwamba mwenye Kufanya Mapenzi killa siku anaondoa uwezekano wa kupata Heart Attack kwa Asilimia 100%

ZIJUE FAIDA ZA KUFANYA MAPENZI

Kiafya
Tendo la ndoa ni moja kati ya mazoezi ya mwili. Wataalamu wanasema kwamba, unapofanya tendo hilo mara tatu kwa wiki husaidia kupunguza kiasi cha mafuta mwilini na pia endapo mtu
atafanya tendo mara tatu kwa wiki kwa kipindi cha mwaka mzima ni sawa na kukimbia maili 75.

Tendo la ndoa huongeza takriban vizalisha nguvu 150 kwa nusu saa ambayo ni sawa na kukimbia dakika 15 kiwanjani.

Kuongeza mwendo wa damu
Tendo la ndoa husaidia kuongeza kasi ya mtiririko wa damu kwenye ubongo na sehemu nyingine ya viungo vya mwili, hii huchangia kuongeza kasi ya mapigo ya moyo na kuboresha mfumo wa upumuaji. Msukumo thabiti wa damu mpya yenye oxygen na homoni zenye chembe chembe hai zinapopenya kwenye mishipa ya damu husaidia katika uunguzaji wa chakula, pia huondoa kiasi cha uchafu ambao ungesababisha mishipa na kushindwa kufanya kazi na kumfanya mwanadamu apate maumivu ya mwili.

Hupunguza mafuta yenye kileo (Cholesterol)
Tendo la ndoa huweka sawa uwiano wa mafuta yenye kileo (Cholesterol) nzuri na cholesterol mbaya na wakati huo hupunguza kwa ujumla kiasi cha mafuta yenye kileo mwilini.

Kupunguza maumivu
Wakati wa kufanya mapenzi, homoni iitwayo oxytosin huzalishwa mwilini ambayo husababisha kuzalishwa kwa homoni iitwayo endorphin ambazo hupunguza maumivu k**a vile kuvimba sehemu za viungo (arthritis) maumivu ya shingo (Whiplash) na maumivu ya kichwa.

Ulinzi wa tezi ya kibofu (mwanaume)Majimaji yanayozalishwa katika tezi ya kibofu (prostate) yakizidi husababisha kuleta matatizo mwilini. Tendo la ndoa la mpangilio huondoa uzalishaji wa majimaji hayo yenye madhara.

Mabadiliko ya ghafla ya tendo la ndoa huelekea kuleta matatizo yahusianayo na tezi ya prostate.

Kupunguza mfadhaiko wa moyo
Kujitosheleza na kupumzisha mwili baada ya tendo la ndoa ni muhimu kwa kutuliza akili na kurekebisha mzunguko wa damu mwilini. Watu wenye kushiriki tendo la ndoa wanatajwa kushinda mfadhaiko na kupata usingizi mnono hasa mara baada ya kumaliza kufanya mapenzi.

Huongeza uzalishaji wa homoni za kiume(testosterone) na za k**e (Oestogen)
Faida nyingine inayopatika ni kuongeza uzalishaji wa homoni za kiume na za k**e likiwemo suala zima la msukumo wa kufanya tendo hilo ambapo mhusika hutosheka zaidi ya yule ambaye hana mazoea ya kufanya mapenzi. Hata hivyo, baadhi ya madaktari wamegundua kwamba ongezeko la homoni za kiume/ k**e huweza kuwakinga wanadamu na magonjwa ya moyo.

Kuishi muda mrefu huku ukionekana kijana
Wakati wa tendo la ndoa homoni iitwayo DHEA huzalishwa mwili mzima. Hii husaidia msisimko wa mapenzi kuongezeka.

Kutokana na elimu hiyo DHEA ni kemikali yenye nguvu duniani ambayo husaidia kuweka sawa kinga ya mwili, huongeza ufahamu, kuimarisha mifupa, kutengeneza na kuimarisha afya na kuimarisha mishipa ya moyo (Cardiovascular).

Hupunguza baridi na mafua
Elimu inaonesha kuwa wanaofanya tendo la ndoa mara moja au mbili kwa wiki huongeza 30% ya uzalishaji wa chembe chembe hai za mwili ziitwazo Immunogloulin A ambazo huwa na kazi ya kuulinda mwili dhidi ya magonjwa.

Hizo ni faida chache tu za kufanya tendo la ndoa.
NB: Jambo kubwa la kuzingatia ni kuwa faida hizi hupatikana kwa ufanyaji wa mapenzi usiokuwa na hofu ya kufumaniwa au kuumbuliwa

HAYA KWA WANA NDOA FANYENI MAPENZI JAPO KWA WIK MARA 3 MUPATE FAIDA ZA TENDO LA MAPENZI NDANI YA NDOA. KWA WALE WASIOWA HAWAPATI HIZI FAIDA SHAURI YENU MSIE OWA OWENI MUPATE FAIDA ZA TENDO LA NDOA

Address

Corner Diwani Street Chang'ombe
Dar Es Salaam

Opening Hours

Monday 16:00 - 00:00
Tuesday 16:00 - 00:00
Wednesday 16:00 - 00:00
Thursday 16:00 - 00:00
Friday 16:00 - 00:00
Saturday 12:00 - 00:00
Sunday 13:00 - 00:00

Telephone

0753192232

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Kyaro cul breeze Pub n Pool. posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share

Category